TUTOE ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI WANAPOKUJA KUPATA HUDUMA ILI KUJIKINGA DHIDI YA MAGONJWA. | Tarimo Blog







Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akifuatilia jarada la moja ya wagonjwa na Mkurugenzi wa uhakiki ubora Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Eliakim Eliud katika hospitali ya mji Karagwe wakati wakiendelea na ziara ya ukaguzi wa hali ya afya katika Mkoa wa Tanga. Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akiwajulia hali wagonjwa wakati wakiendelea na ziara ya ukaguzi wa hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Tanga.Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akifuatilia utoaji huduma katika dirisha la wateja wa maabara katika hospitali ya mji Karagwe wakati wa ziara ya ukaguzi wa hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Tanga.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akiongozana na Mkurugenzi wa tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Maghembe katika eneo la mapokezi hospitali ya mji Karagwe wakati wakiendelea na ziara ya ukaguzi wa hali ya afya katika Mkoa wa Tanga.


*************************************

Na WAMJW- TANGA

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameagiza Watoa huduma za Afya nchini kutoa elimu ya Afya kwa wananchi, pindi wanapofika kupata huduma, ili kupata ujuzi wa namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa katika Jamii.

Agizo hilo amelitoa leo, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya kwa wananchi katika Hospitali ya mji ya Korogwe ikiwa ni muendelezo wa ziara yake iliyoanza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga.

“Nitoe wito kwenu, kutoa elimu ya Afya kwa wananchi wanaokuja kupata huduma za Afya na wale wanaowasindikiza wagonjwa kupata huduma, hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kujikinga dhidi ya magonjwa katika jamii yetu” alisema Prof. Makubi.

Pia, Prof. Makubi ametoa wito kwa viongozi kuongeza jitihada katika mapambano dhidi ya vifo vya wajawazito, kwa kutoa mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya chini jinsi ya kutatua changamoto kipindi cha kumuhudumia mjamzito.

Aidha, Prof. Makubi ametoa wito kwa viongozi kubuni mbinu tofauti za kuongeza mapato ya ndani, na kuondokana na fikra za kuitegemea Serikali kuu kuwaletea mapato, huku akisisitiza kufanya hivyo kutachangia utoaji huduma bora na kuboresha maslahi ya Watumishi.

“Tunafahamu hali ya uchangiaji wa wananchi ni mdogo, lakini ni lazima tujiongeze ili kuongeza mapato na tuweze kujiendesha wenyewe kama Hospitali, tusisubiri kila kitu kusaidiwa kutoka Serikali kuu,” alisema Prof. Makubi.

Hata hivyo, Prof. Makubi ametoa wito kwa Hospitali kuwatumia wataalamu wa Afya wanaojitolea (volunteers) walio na vigezo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana dhidi ya changamoto ya Watumishi wakati Wizara ikingoja kibali cha ajira kutoka utumishi.

Kwa upande mwingine, Mganga Mkuu wa Mji wa Korogwe Dkt. Elizabeth Nyema, amesema kuwa, hali ya utoaji chanjo katika mji wa Korogwe ni asilimia 97.6% ( penta 100%, MR – 61%, na HPV1 – 90%, na HPV2 – 89%), huku akiweka wazi kuwa, kwa kiasi kikubwa hali muitikio wa kupata chanjo kwa wananchi upo vizuri.

Mbali na hayo, amedai kuwa, kama viongozi wamefanikiwa kuanzisha kitengo cha kutoa matibabu kwa watoto wenye utapiamlo mkali kwa kutengeneza chakula dawa (F75 na F100), huku watoto 84 wamefanikiwa kupata matibabu hali iliyosaidia kupunguza Rufaa katika Hospitali ya Mkoa ya Tanga – Bombo.

“Tumefanikiwa kuanzisha kitengo cha kutoa matibabu ya watoto wenye utapiamlo mkali, octoba 2019, katika wodi kwa kutengeneza chakula dawa (F75 na F100), na Tumefanikiwa kutoa matibabu kwa watoto 84 na hii imesaidia sana kupunguza rufaa za watoto hawa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tanga – Bombo” alisema.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2