JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU 4 KWA TUHUMA ZA MAKOSA YA KUPANGA TUKIO LA MAUAJI YA MTU MMOJA WILAYANI UKEREWE.
TAREHE 25.08.2020 MAJIRA YA 02:00HRS USIKU ENEO LA MISSION, KATA YA NYAMANGA, KISIWA CHA UKARA, WILAYA YA UKEREWE, MKOA WA MWANZA, ANDREW MAGAI, MIAKA 48, MKARA, MKRISTO, MKULIMA WA KIJIJI CHA CHIBASI, ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA KUKATWA NA VITU VINAVYODAIWA KUWA NA NCHA KALI KWA MADAI KUWA MAREHEMU KABLA YA KIFO CHAKE ALIWASAFIRISHA WATU AMBAO HAWAKUTAMBULIKA KWENDA KUVUNJA NYUMBA YA MAGESA SIMON @ WILE.
UCHUNGUZI WA AWALI UMEBAINI KUWA TUKIO LA KUVUNJA NYUMBANI KWA MAGESA SIMON @ WILE LILIKUA NI LA KUTENGENEZWA ILI KUHALALISHA MAUAJI YALIYOTOKEA ENEO HILO. UCHUNGUZI WA KINA UNAENDELEA UKIHUSISHA WATAALAMU MBALIMBALI. MWILI WA MAREHEMU ULIFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI KATIKA KITUO CHA AFYA BWISYA NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU KWA MAZISHI.
WALIOFIKISHWA MAHAKAMANI LEO 31/08/2020 NI:-
-
MAGESA SIMON @ WILE, MIAKA 50, MKALA, MKULIMA, MKAZI WA NYAMANGA.
-
MAKANJE MGETA, MIAKA 28, MKARA, MKAZI WA KIJIJI CHA CHIBASI.
-
MKAPA MAGESA@SIMON, MIAKA 24, MKARA, MKULIMA, NYAMANGA.
-
SELESTINI DATUSI, MIAKA 22, MKEREWE, MKRISTO, MKULIMA, NYAMANGA.
WATUHUMIWA WOTE WAMEFIKISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KUJIBU TUHUMA ZINAZOWAKABILI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKA WANANCHI, WANASIASA WA VYAMA VYOTE KUTOJIINGIZA KATIKA MAMBO AMBAYO YANAWEZA KUHAMASISHA UVUNJAJI WA SHERIA NA KUVURUGA AMANI NA UTULIVU WA NCHI, LIMEAPA KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KALI KWA KILA ATAKAYEKIUKA SHERIA.
IMETOLEWA NA:-
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
31 AUGUST, 2020
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment