AMNESTY INTERNATIONAL YATAKA UCHUNGUZI HURU KATIKA MAUAJI | Tarimo Blog

Na Lusajo Frank, Michuzi TV
SHIRIKA la Kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limetoa wito wa uchunguzi huru katika kisa ambapo mwanamke mmoja aliuwawa akiwa uchi huko nchini Msumbiji.

Taarifa zinasema kwamba mwanamke huyo aliuwawa na wanaume waliokuwa wamevalia sare za kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo eneo lililokuwa na machafuko. 

Haya yanajiri wakati ambapo serikali ya Msumbiji inajaribu kujiondolea lawama kwa kuwanyoshea kidole cha lawama magaidi ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi katika mkoa wa Cabo Delgado.

Kuliibuka mkanda wa video wiki hii uliowaonyesha wanaume waliovaa sare za kijeshi wakimpiga mwanamke waliyemtuhumu kwa kuwa mwanamgambo na kisha baadae kummiminia risasi. Serikali imesema itauchunguza mkanda huo wa video.

"Wanajeshi wanne tofauti walimpiga risasi jumla ya mara 36 na aina ya bunduki za Kalashnikov na bunduki aina ya PKM," Amnesty ilisema, ikitaka "uchunguzi huru ufanyike".

"Video hii ya kutisha bado ni mfano mwingine mbaya wa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji yasiyo na huruma yanayofanyika Cabo Delgado na vikosi vya usalama vya Msumbiji," alisema Deprose Muchena, Mkurugenzi wa Amnesty International kwa Mashariki na Kusini mwa Afrika.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2