Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akitoa mada katika Mafunzo ya Wakurugenzi vijana kutoka Kampuni mbalimbali hapa nchini yanayofanyika katika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.
Mhadhiri Mwandamizi kutoka shule ya biashara Chuo Kikuu Mzumbe na Mkurugenzi mwenza kutoka Bodi ya wakurugenzi wasomi Tanzania Dkt. Emmanuel Chao akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wakurugenzi vijana kutoka Kampuni mbalimbali yanayoendelea kufanyika katika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam na kutamatishwa Septemba 11, 2020.
Baadhi ya Wakurugenzi vijana kutoka Kampuni mbalimbali hapa nchi wakisikiliza mada.
Washiriki wa mafunzo ya Wakurugenzi vijana kutoka Kampuni mbalimbali hapa nchini wakimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea katia Chuo Kikuu Mzumbe, Dar es Salaam.
Wakurugenzi vijana kutoka Kampuni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi na Mhadhiri Mwandam kutoka shule ya biashara Chuo Kikuu Mzumbe na Mkurugenzi mwenza kutoka Bodi ya wakurugenzi wasomi Tanzania Dkt. Emmanuel Chao.
Mhadhiri mwandamizi kutoka Shule ya biashara Chuo Kikuu Mzumbe na Mkurugenzi mweza kutoka bodi ya wakurugenzi ya wasomi Tanzania, Dkt Emmanuel Chao akizungumza mara baada ya semina kwa Wakurugenzi vijana inayofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam amesema kuwa mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwaanda wakurugenzi vijana kuweza kujua namna ya kusimamia Kampuni zao.
"Lengo kuu la Mafunzo haya ni kuwawezesha Wakurugenzi vijana kuongoza kampuni kitaalamu kwa miaka 10 hadi 20 ijayo katika Taifa." Amesema Dkt. Chao.
Dkt. Chao amesema kuwa mafunzo hayo yana maono makubwa ya kuwafikia vijana wengi zaidi ambao wameshaanza kusimamia kampuni zao.
Hata hivyo Dkt. Chao amesema kuwa leo wameanza kutoa mafunzo ya namna ya kusimamia uongozi wa bodi katika Kampuni mbalimbali na namna ya kuongoza bodi kwa njia ya mitandao mbalimbali na namna ya kusimamia bodi hizo.
"Mada ya leo ilikuwa muhimu sana kwa Wakurugenzi vijana katika kusimamia Kampuni ambazo ndio zimeanza kwa kuunda bodi, usimamizi, wa bodi pamoja na utekeleza wake". Amesema Dkt. Chao
Dkt Chao ametoa wito kwa wakurugenzi vijana kushiriki mafunzo hayo kwa wakati yatakapo tangazwa kwani ni mhimu hasa kwa kampuni zinazoanza.
Miongoni mwa watoa maada katika Mafunzo hayo, Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaa ya Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Ngowi amesema kuwa wakurugenzi Vijana wanatakiwa kwenda na Teknolojia kwani huwezi kukusanya watu wengi katika sehemu moja badala yake wanaweza kutumia mkutano kwa njia ya video.
Kwa upande wa Washiri wamepongeza waandaji wa mafunzo hayo kwa yata wasaidi saha hasa pale wanapotaka kuunda bodi ya wakurugenzi kwa ajili ya kusimamia na kutekeleza mikakati watakayojiwekea.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment