COSTECH YAANDAA MIONGOZO KURATIBU UTAFITI NCHINI | Tarimo Blog

Na Karama Kenyunko Michuzi TV.

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imeandaa miongozo mingine ya kuratibu masuala ya utafiti nchini kwa ajili ya watafiti waliopo na watafiti watarajiwa na kupeleka kwa wadau wa elimu kuonesha nankuigawa kusudi iweze kuwaongoza.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Amos Nungu ameyasema hayo leo Septemba 5,2020 wakati wa kufunga Maonesho ya 15 ya vyuo Kikuu yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya sherehe za kufunga Maonesho hayo Dkt. Nungua amesema Costech kama Tume ambao imekuwa ikiratibu sayansi na Teknolojia hapa nchini pia inaratibu ngazi za elimu ya juu kwa maana ya watafiti, wabunifu na waliopo kwenye utafiti Maendeleo.

"Tumekuwa hapa viwanjani kwa wiki nzima, kazi yetu, ilikuwa ni kuandaa miongozo majarida na kutoa elimu na ushauri kwa wadau washiriki jambo ambalo tunashukuru mungu limeenda salama" amesema Dkt. Nungu

Amesema, Teknolojia na ubunifu ni suala mtambuka lakini pia mazingira yake hubadirika kila wakati, zamani google haikuwepo lakini sasa ipo, hivyo hata uratibu unabadirika kutokana na mazingira kwani mwaka 2018 tulifanikiwa kuandaa muongozo wa kutambua wabunifu na wagunduzi hapa nchini ingawa kabla ya hapo tulikuwa tunafanya lakini hakukuwa na muongozo rasmi.

"Kwa mfano sisi tunaratibu masuala ya kutoa vibali vya utafiti hapa nchini. Pale tunamiongozo ambayo inakiri kwamba Costech kama Taasisi tunaratibu. Watendaji wako vyuoni inabidi tuwasaidie kuwaongoza ili nao waweze kufanya vizuri. Poa miongozo hiyo tunaitumia kuwajengea kule kamati za kusaidia kufanya mapitio ya maombi kusudi mwishoni yanapokuja Costech kwa ajili ya kupata kibali yawe yameishachakatwa. Maana tukisema costech ifanye kazi zote, tutakuwa tunachelewesha kazi", amesema Dkt. Nungu.

Aidha Dkt. Nungu amezipongeza Taasisi zilizofanya udahili wa wanafunzi pale pale viwanjani na kuongeza kuwa hiyo ni Faraja kubwa kwa Costech maana mwaka jana kulikuwa na vyuo viwili tu vilivyokuwa vinatoa huduma hiyo lakini safari hii vyuo vyote vimetoa huduma hiyo uwanjani hapo kwa kutumia Teknolojia huku pia baadhi ya Taasisi zikionyesha Ubunifu wao ambao wametengeneza vyuon

Pia ameongeza kuwa, mwamko kwa vijana wanaofanya utafiti ni mkubwa lakini pia unachangamoto zake, kwa sababu ubunifu unazidi kukua siku hadi siku. Amesema  vijana wengine ni wajasiriamali anaenda na kusema anawazo la ubunifu na anaomba hela lakini ki ukweli wazo lake ni la kumsaidia kumuongoza na siyo la pesa sasa mpaka uje umbadirishe kuwa hilo wazo lako halihitaji hela ni kazi.

"Lakini kuna wengine wana bunifu ambazo ni nzuri kuziona kwa macho yaani ni bunifu kwa ajili ya Maonesho lakini zile ukishabuni mwisho wa siku inatakiwa ziende kwenye jamii zikatumike, sasa kwa kuangalia ni nzuri tunawapigia makofi lakini kwenye jamii nani yuko tayari kulipa kusudi aweze kuitumia hawapo hivyo tunaendelea kuwajengea uwezo, kuandika vipeperushi ili kuwaongoza kwamba ubunifu ya namna hii ni mzuri lakini je unatatua changamoto au ubunifu wake unawezekana kwamba kwa mazingira ya ulaya unafaa lakini kusudi uwe na maana inabidi  utumike.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Amos Nungu 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2