Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Urambo
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa amewaahidi wakulima wa zao la Tumbaku katika Mkoa wa Tabora kwamba changamoto zilizopo katika zao hilo zitapatiwa ufumbuzi.
Amesema ndio maana ameamua kumteua Hussein Bashe anayetoka mkoa huo kuwa Naibu Waziri wa Kilimo ili aanze kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo.
Akizungumza leo asubuhi na wananchi wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora,Dk.Magufuli amesema kuwa anajua kuna changamoto kadhaa ambazo wakulima wa zao la Tumbaku wanakumbana nazo ikiwemo changamoto ya soko la tumbaku.
Dk.Magufuli amefafanua kuwa wakulima wa zao hilo wanajitahidi kulima kwa bidii lakini wanakosa wanunuzi na hata bei ambayo wakati mwingine wanauza inakuwa iko chini na malipo yanachelewa.
"Nawaomba niwahakikishie wananchi wa Urambo na Mkoa wa Tabora kwa ujumla changamoto hizi tumezibabe na tutatafuta ufumbuzi wake,"amesema Dk.Magufuli na kusisitiza Bashe alimteua ili afuatilie na kujua chanzo cha matatizo hayo ya wakulima wa tumbaku.
Hata hivyo amesema bei ya masoko mengi ya mazao kama pamba, tumbaku na korosho ilishuka kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona na hivyo kusababisha wazungu ambao ni wanunuzi kujifungia ndani, ndege, meli zilikuwa hazisafiri.
"Sasa utapeleka wapi wakati wanunuzi wamejifungia?Halafu wanatokea watu wanasema Serikali haitaki kununua tumbaku walipaswa waseme ukweli kuwa mambo yamevurugika kule maana Corona".
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment