DKT. MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA | Tarimo Blog

Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nzega mkoani Tabora katika Kampeni za Urais za CCM wakati katika Uwanja wa Parking mjini Nzega leo Jumatano Septemba 2, 2020.
Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ilani ya Uchaguzi iliyo kubwa mara tatu na ya Uchaguzi Mkuu uliopita wakati kizungumza na Wananchi wa Igunga mkoani Tabora katika
Kampeni za Urais za CCM akiwa njiani kuelekea Nzega leo Jumatano Septemba 2, 2020.
Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea nafasi za Udiwani wakati kizungumza na Wananchi wa Igunga mkoani Tabora katika Kampeni za Urais za CCM akiwa njiani
kuelekea Nzega leo Jumatano Septemba 2, 2020.


*Asema matusi mengi anayotukana kwake ni furaha, ndio sadaka yake kwa Watanzania

*Aomba tena miaka mitano afanye maajabu , Tanzania iwe kama Ulaya


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Nzega

MAELEFU ya wananchi wameendelea kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya mgombea urais wa Serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli huku akitumia nafasi hiyo kuelezea kwamba iwapo atapa miaka mitano mingine ya kuongoza nchi anataka kufanya maajabu kwa maendeleo ambayo atayaleta kwa Watanzania.

Hata hivyo amesema pamoja na nchi yetu kupata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano, bado kuna watu wameendelea kumtukana matusi mengi ya kila aina kwake hiyo ndio sadaka yake kwa Watanzania kwani dhamira yake ni kuona nchi inakuwa na maendeleo na ifike wake Tanzania iwe kama Ulaya kupitia miradi inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na wananchi wa Nzema Mjini mkoani Tabora leo Septemba 2, mwaka 2020 katika Uwanja wa Parking ,Dk.Magufuli ameelezea sababu zinazomfanya yeye na Chama chake cha CCM kurudi tena kwa wananchi kuomba ridhaa ili katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 wamchague akafanye kazi ya kuleta maendeleo ambapo ameeleza kwa kina maendeleo yaliyopatikana kwa miaka mitano.

“Tumepata maendeleo makubwa katika nchi yetu, kazi yangu ninayoifanya ni sadaka kwa ajili ya Watanzania, matusi ninayotukwana kwangu nafurahi, ndio maana nasema muendelee kuniombea maana waliokuwa wanatuibia hawawezi kufurahi ndio maana matusi yote yanakuja kwangu.

“Acha mimi nitukanwe lakini ninyi mpate maendeleo na ndio maana nimekuja hapa kuomba tena kura, naomba kura za watu wa Chadema, ACT, NCCR-Mageuzi, CUF na hata na wasio na vyama wote naombeni kura zenu,”amesema Dk.Magufuli wakati akielezea namna ambavyo kuna watu wasioitakia mema nchi yetu ambavyo wanakasirishwa na kazi inayofanywa na Serikali ya kuleta maendeleo lakini hajali na ataendele kuchapa kazi.

Wakati huo huo Dk.Magufuli amesema tangu ameingia madarakani hajawahi kwenda Ulaya na kwamba alienda Ulaya wakati alipokua akisoma na kwake huo ni ushujaa huku akisisitiza kwamba nchi yetu itapata maendeleo makubwa na haitakuwa na tofauti na nchi za Ulaya.

Wakati akielendelea kuzungumza na wananchi hao ,Dk.Magufuli amesema kuwa iwapo atapa tanasi ya miaka mitano mingine atafanya maajabu makubwa katika kuleta maendeleo zaidi ya ilivyofanyika sasa.”Nipeni nafasi nyingine, natafaka kufanya maajabu , katika hili nawaahidi, ndio maana nimekuja kuomba kura tena kwa mara nyingine.”

Kuhusu Mkoa wa Tabora amesema miaka ya nyuma mkoa huo ambao ni miongoni mwa mikoa mikubwa ulikuwa na changamoto nyingi lakini imefanyika kazi kubwa ya kuleta maendeleo na wananchi wa Mkoa hu wanafahamu hali iliyokuwepo huko nyuma, ambapo kulikuwa na changamoto za kila aina kuanzia barabara, miundombinu ya afya, elimu na maji na huduma nyingine zilikuwa duni.

“Kwa hapa tu Wilaya ya Nzega mradi mkubwa maji kutoka ziwa Victoria unakwenda kunufaisha watu 55000.Tumetumia fedha nyingi kwa ajili ya mradi huo, kuna watu ambao hawakuwa wakitarajia kama kuna siku maji yatatoka Ziwa Victoria kuja Tabora na Nzega ,Igunga na maeneo mengine lakini tunaifanya kazi hiyo ya kutatua changamoto ya uhaba wa maji,”amesema Dk.Magufuli.

Amefafanua kuwa mradi huo wa maji utanufaisha watu wote kwani watakunywa maji hayo.”Nipo kwa niaba ya Watanzania wote na ndio maana nawaomba kwa upendo mkubwa mnirudishe tena, mtaona maajabu.

Akielezea zaidi mkoa huo wa Tabora amesema mkoa huo mkubwa lakini ulikuwa haujanganishwa kila tukiomba fedha kwa wafadhili hakuna aliyekubali hadi tulipoamua kutumia fedha zetu wenyewe, ukitoka Tabora kwenda Kigoma zimebaki kilometa 50,Tabora hadi Mpanda kilometa 359 na makandarasi watatu wanaweka lami, hivyo atashangaa kama haya yote ambayo nimefanya shukrani yake n kunyimwa.

Amesema katika kilimo, amesema kuna jitihada mbalimbali zinaendelea kuhakikisha kilimo kinapewa mkazo zaidi na katika kipindi cha miaka mitano wataendelea kuiboresha sekta hiyo.”Naibu Waziri wa Kilimo ni Hussein Bashe ambaye anatoka hapa Nzega mnamuona ambavyo anahangaika katika kufanya kazi.”

Kuhusu mapokezi aliyoyapata amesema amepita katika maeneo mbalimbali lakini Nzega imefunika kwani mtu huwezi amini kama uko kwenye wilaya.

Pia amesema wapo wanaosema Tanzania ni nchi masikini lakini yeye anawaambia nchi ni matajiri na mambo mengi yamefanyika.”Sisi tumenunua ndege 11 mpya, wanaohoji kuhusu ndege wamechanganyiwa, ukiwa na ndege ndio unasafirisha dawa, hata ukiwa na bajaji huwezi kuleta dawa kutoka ulaya.”

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2