Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Imetoa tuzo Kwa wanafunzi na walimu bora kitaifa waliofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia, Fizikia na Baiolojia kidato cha Nne na Kidato cha sita kwa mwaka 2018.
Akizungumza wakati wa kutoa tuzo hizo jana jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia ,Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe amesema kuwa Tuzo hizo zinatoa uwigo kwa wanafunzi kipenda masomo ya Sayansi na baadae kupata wataalam wataotumikia Taifa.
Profesa Mchembe amesema kuwa GLCA kuendelea kutoa tuzo hizo kwa kuongeza masomo kwani wametambua masomo hayo yanavyotegemeana.
Aidha amesema kuwa kutokana na Tanzania kuongia uchumi wa kati GCLA kwa kushirikiana na vyuo kuanza kutengeneza vitu vya maabara na uwezo huo unawezekana.
Profesa Mchembe, aliwataka wazazi na kuwaamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kuhimizwa kupenda masomo ya Sayansi lakini pamoja na kuhimiza shuleni kunatakiwa kuwepo na vifaa vya kufanyia mazoezi.
"Mashuleni kunatakiwa kuwepo na vifaa vyote vya msingi ili kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri na kuwa na uwelewa juu ya kitu wanachofundishwa na sio wanafunzi kujifunza darasani bila vitendo huku mkitegemea wanafunzi kujuwa kwa kusikia wanatakiwa kuona wanachoambia.
"Tumeingia kwenye uchumi wa kati kwa hiyo ushindani ni mkubwa wanafunzi wanatakiwa kusoma kwa bidii, kwa vitendo zaidi katika kuwa na wataalam wanaongia katika ushindani katika soko la ajira.
"Napongeza Wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi wanavyopewa kipaumbele kwenye mikopo kwani wanawatia moyo wanafunzi kupenda masomo hayo "amesema Profesa Mchembe
Nae Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fedelice Mafumiko amesema zawadi na Tuzo wanazozitoa ni kusaidia wanafunzi kuwapa motisha katika kusoma kwa bidii pamoja na walimu kuongeza bidii katika ufundishaji.
Dkt.Mafumiko amesema walianza kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye somo la kemia lakini tukaongeza wigo kwa masomo ya Baiolojia na Fizikia.
"Tuzo za kupongeza walimu na wanafunzi hadi sasa wamefika wanafunzi 128 walimu 22 .
Amesema Shule kwa Kidato cha Nne zilizofanya vizuri na kuongoza katika masomo ya Kemia, Baiolojia na Fizikia, ni St.Francis wanafunzi 8, St Anne, St.Mary's Ilboru, Kilakara Tabora Girl, Feza.
Wanafunzi waliopata tuzo ni Maria Manyama, Kutoka St Francis, aliyeshika nafasi kwanza kwenye somo la Kemia ya kitaifa 7 Atunganile Mlinga kutoka St Francis, Samira Kishashu kutoka Bright Future Girls 15, wanaume ni John Marian Boy's 1, kemia, Rahim Tulingwa 2 Marian Boy's Marian Boy's 3
Maria Manyama biologia nafasi ya pili kitaifa St Francis, Nancy Yolanda kutoka St Francis, Ahmad Edwin Kachenje, Msolwa nafasi ya pili kitaifa Frank Christian,
Rolete Len, Braison, Miayo Saidi .
Waliofanya vizuri kidato 6
Glory Patson1, 2 kitaifa, Naomi Tundui 2' kitaifa 5
Kwa niaba ya wazazi Norbet Leone amesema kuwa tunawapongeza na kuwashukuru walimu kwa kuweza kuwasaidia watoto wetu kwa kuwapa mafunzo na kuweza kufanya vizuri.
"Pamoja na kuwa na niwapongeze wanafunzi kwa kusoma kwa bidii na kuweza kufanya vizuri kama wazazi tunajisikia fahari katika hilo mlilolifanya hongereni"amesema Leone
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akikabidhi Mzazi wa Mwanafuzi aliyefanya vizuri katika somo la Fizikia Norbet Leone katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe akizungumza na Wazazi na Wanafunzi katika utoaji wa Tuzo za Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika Masomo ya Kemia,Baolojia pamoja Fizikia kwa matokeo ya Kidato cha Nne na Sita Tuzo hizo hutolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) halfla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko akizungumza kuhusiana utaratibu wa utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika matokeo ya Kidato cha Nne na Sita katika masomo ya Kemia,Baolojia pamoja na Fizikia katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA ) Profesa Esther Hellen Jason akizungumza kuhusiana na watoto wa kike kupenda masomo ya sayansi katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi matokeo ya Kidato cha Sita na Nne katika masomo ya Kemia,Baolojia na Fizikia.
Mwakilishi wa Wazazi w a Wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya Kidato cha Sita na Nne katika masomo ya Kemia ,Baolojia pamoja na Fizikia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Profesa mabula Mchembe akiwa katika picha ya pamoja Wazazi,Walimu katika Hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment