Mgombea udiwani kata ya Manda Efrida Kilumbo akiwa amepiga magoti kuwaomba wananchi kumpigia kura katika uchaguzi mkuu October 28.
Mwenyekiti wa CCM wilaya stainley Kolimba akiongea na wananchi wa kata ya Manda wakati wa uzinduzi wa kampeni katika kata hiyo.
Kikundi Cha ngoma ya kihoda, ikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni katika kata ya Manda.
Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume, akizungumza na wananchi wa kata ya Manda iliyopo wilayani humo mkoani Njombe.
Mgombea udiwani kata ya Manda Efrida Kilumbo (kushoto) akicheza ngoma ya kihoda
Aliyekuwa mbunge viti maalum Dk. Susan Kolimba, akiongea na wakazi wa kata ya Manda ( hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni katika kata hiyo.
===== ======== ======== ==========
Na Shukrani Kawogo, Njombe
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Bakari Mfaume amesema kuwa hawatapoteza muda kujibu hoja zisizo za msingi kutoka kwa vyama pinzani kwakuwa wanamambo mengi ya msingi ya kuzungumzia juu ya utekelezaji wa ilani ya chama.
Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa kampeni katika kata ya Manda uliofanyika katika kijiji cha Nsungu wilayani Ludewa mkoani Njombe na kuongeza kuwa vyama pinzani havina mambo ya kusema katika majukwaa yao na ndio maana wanaamua kuanza kukizungumzia chama tawala pamoja na kusema mtu mmoja mmoja katika chama.
Alisema kuwa ni dhahiri kabisa wapinzani wamekosa vya kuzungumza juu ya sera zao pamoja na ahadi juu ya kile watakachowafanyia wananchi katika kipindi cha miaka mitano na ndiomaana wanaanza kuzungumza mambo ya uongo juu ya chama tawala.
“Mambo yaliofanywa na chama chetu ni mengi sana kiasi kwamba hatuwezi kuyamaliza kuyazungumza hivyo hatuwezi kupoteza muda wetu kuwazungumzia wao wakati yapo mambo ya msingi sana ya kuzungumza na ni wazi kuwa hata wakipewa uongozi hakuna watakachoweza kukifanya”. Alisema Mfaume.
Naye liyekuwa Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Njombe Dk. Susan Kolimba amewataka wabunge wa majimbo yote ya mkoa huo kupitia chama hicho watakaochaguliwa na wanachi kuingia bungeni kuwa na umoja ili kuleta maendeleo katika majimbo hayo.
Dk. Suzan ambaye pia aligombea nafasi ya ubunge katika kura za maoni ndani ya chama hicho lakini kura zake hazikutosha ambapo Joseph Kamonga ndiye aliyeibuka mshindi katika nafasi hiyo huku Dk. Susan akishika nafasi ya tatu.
Aliongeza kuwa viongozi wanapokuwa na umoja huleta matokeo mazuri katika maendeleo hivyo licha ya kushirikiana wao kwa wao pia wanapaswa kushirikiana na vyama vyao ambavyo vimewateuwa katika kutimiza ilani ya chama hicho.
“Katika kuleta maendeleo hakuna kitu kizuri kama ushirikiano hivyo wabunge hawa wakiwa na ushirikiano wa kutosha na viongozi wa chama, serikali na hata kwa viongozi mbalimbali waliopita ili kuwashauri mambo mbalimbali wataweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana katika kuleta maendeleo”. Alisema Dk. Suzan.
Aidha kwa upande wa mgombea Udiwani wa kata hiyo Efrida Kilumbo amewaomba wananchi wa kata hiyo kumpa tena ridhaa ya kuwaongoza huku akiwaahidi kuendelea kuwa mwaminifu katika kutekeleza iklani ya chama hicho.
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita amefanya mambo mengi ya maendeleo jatika kata hiyo hivyo anawaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kumuamini ili aendeleze miradi mbalimbali ambayo bado haijakamilika.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment