Mmoja wa wana jeshi akimsogeza mlevu katika eneo la picha ya pamoja wakati kikosi hicho cha jeshi la wananchi kilipofika kwa ajili ya kutoa msaada.
Baadhi ya vitu vitu vilivyotolewa na jeshi la wananchi kwa kituo cha Inuka.
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katika kuadhimisha miaka 56 ya jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania hii leo Septemba 1,2019. Kikosi cha 514 Makambako kimetoa msaada wa vitu mbali mbali katika kituo cha kutibu watu wenye ulemavu wa viungo cha Inuka wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe Pamoja na kuchangia damu katika kituo cha afya cha Jeshi mjini Makambako.
Meja Iddi Sechonge kaimu kamanda kikosi cha jeshi la ulinzi wa wananchi kikosi cha 514 Makambako akikabidhi misaada hiyo katika kituo cha Inuka amesema kuwa jeshi linaadhimisha kuanzishwa kwake kwa kutoa misaada katika jamii inayolizunguka ili kuwasaidia wasiojiweza.
“Tunaadhimisha kuanzishwa kwa jeshi letu,kwa maana tumeona tushehereke na kituo hiki kwa ajili ya kuwapa chochote,lakini kuna wenzetu wanaendelea na zozi la kuchangia damu”alisema Meja Iddi Sechonge
Kaimu mkurugenzi wa kituo cha Inuka Dokta Salehe Abdalaha amesema kuwa jamii bado inaimani potofu dhidhi ya watu wenye ulemavu Pamoja na kueleza kuwa misaada zaidi inahitajika kwa kuwa baadhi yao hushindwa kumudu gharama za matibabu.
“Kuna changamoto ya uelewa kwenye jamii na baadhi yaw engine wanadhaani ni laana lakini sisi tunachosema mtu anaweza akapata uleamvu saa yoyote”alisema Dokta Salehe Abdalaha
Zaidi ya uniti 35 za damu zimepatikatikana katika kituo cha afya cha jeshi la ulinzi wa wananchi kikosi 514 Makambako Mkoani Njombe
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment