Na Said Mwishehe, Michuzi TV -Tabora
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Dk.John Magufuli amekuwa akilala saa chache sana kwa ajili ya kuwaza na kupanga mipango ya maendeleo kwa ajili ya Watazania wote.
Hata hivyo amesema kuna wapinzani wamekuwa wakimpaka matope na kumchagua Dk. Magufuli, hivyo amewaomba wananchi wawapuuze na wala wasiwasikilize.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Tabora ambao waliofika katika mkutano wa kampeni za Dk.Magufuli ambaye amefika katika mkoa huo kuomba ridhaa ya kchaguliwa tena kuwa Rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
"Dk.John Magufuli ni mtu mpenda nchi, analala saa chache kwa ajili ya kuwaza na kupanga maendeleo ya nchi hii, Tabora sote ni mashahidi nchi hii inasonga mbele kwa spidi kubwa, tunaomba tumchague mgombea urais wa CCM kwa ajli ya maendeleo yetu.Nawaomba mumchague mgombea ubunge wa Tabora Mjini Emmanuel Mwakasaka
"Baadhi ya wagombea ubunge walikuwepo bungeni, Rais alipoleta bajeti ya barabara, maji umeme kwa ajili ya Tabora wao wao walipinga.Kura zote ziende kwa mgombea Dk.John Magufuli ili arudi kwenye nafasi yake,"amesema Ndugai.
Awali wakati akianza kuzungumza alisifu idadi kubwa ya wananchi wa mkoa huo waliojitokeza uwanja huo mkubwa wa Ali Hassan Mwinyi uliopo mkoani Tabora.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hassan Mwakasubi amesema Kamati Kuu iliwapa maelekezo ya kufanya kampeni za kistaarabu lakini wanasiasa wa vyama vya upinzani wamekuwa wakitoa maneno ya shombo na yanayokera.
"Wanabeza kazi nzuri ambayo imefanywa na Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano. "Sasa imetosha, tunataka nao wajue kachumbari ni mboga au saladi.Wanaosema maneno ya kubeza nasi tutaanza kuwajibu na ukiona mchwa anakula mpini ujue anamtafuta mwenye jembe.
"Makaribisho ya leo Tabora haijahi kutokea, tunajivunia mafanikio katika miaka mitano, Tabora leo inaitwa Toronto, miradi mingi imefanyika, wengi wameongelea maji, umemtua ndoo mama kichwani, kuhusu umeme umekwenda katika vijiji mbalimbali na vile ambavyo havijapata umeme umetuhakikisha tutawekewa.Tunashukuru pia yaliyofanyika katika sekta ya afya ni makubwa sana,"amesema.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Spika wa Bunge Job Ndugai
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment