Hii ni hatua nyingine thabiti iliyochukuliwa na Tanzania kuelekea kuimarisha uwezo wake wa kuhamia dijitali.
Katika mafunzo hayo ya teknolojia ya 5G ambayo yametolewa na Kampuni ya Huawei Tanzania yamehusisha kundi la kwanza la wataalamu wa Kitanzania, ambao wamechukua kozi muhimu ya teknolojia za redio za 5G na upelekaji wa mtandao, mahitaji ya wigo wa 5G na upangiliaji, modeli za biashara za 5G na usimamizi wa 5G.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti hivyo iliyofanyika mapema hii leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk Zainab Chaula, awapongeza wahitimu wa mafunzo hayo pamoja na Kampuni ya Huawei Tanzania akibainisha kuwa Serikali imedhamilia kuongeza uwekezaji kwenye nyanja ya dijitali.
“Tunahitaji kwenda na wakati na kujifunza maarifa na ujuzi wa kisasa ambao unakidhi mahitaji ya enzi hii ya dijitali na kuwa makini na mifumo ya kisasa ambayo inaweza kubadilisha au kuvuruga biashara na maisha yetu. Jambo la muhimu zaidi tunahitaji kuimarisha ustadi wetu kwenye TEHAMA kupitia mafunzo na uwezeshaji mpya ili kuendana na kasi ya mabadiliko, kukabiliana na changamoto na kuwahudumia watu wetu kwa ubunifu na ufanisi."Alisema Dk Chaula.
Aidha, Dk Chaula alisema mafunzo haya yaliyotolewa na Huawei ni mfano mzuri wa jinsi taifa linavyoweza kufanikiwa kwa kufanya kazi na wadau binafsi wa kuaminika katika kuimarisha uwezo wake.
“Uwekezaji huu umekuja wakati muafaka kwa kuwajengea uelewa wa kidigitali Watumishi wa umma, na kwa kiwango kikubwa itasaidia uboreshaji wa jukwaa la huduma za Kiserikali kidijitali, moja wapo ya vitu vitatu muhimu vya Programu ya Dijitali ya Tanzania (DTP). Ni muhimu kwetu kukuza mazingira wazi na mfumo wa ikolojia ambapo kila mdau anaweza kushiriki, kuchangia, na kufaidika nayo, na ambayo itasababisha ukuaji endelevu wa sekta na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.’’ Alisema
Alisema serikali inakaribisha washirika kama Huawei kushiriki zaidi katika majadiliano, kujenga uwezo na mashauriano ya sera juu ya jinsi ya kukabiliana na changamoto na kutumia fursa ya kuelekea Uchumi wa kati, na kutoa mchango wao katika ustawi wa taifa kidigitali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bw. Damon Zhang alisema tangu kuanza shughuli zake nchini mnamo mwaka 2007, Huawei Tanzania imejitolea kufundisha maarifa na ustadi wa TEHAMA kwa watanzania, na wataalamu wote kwa kuwajengea uwezo na utaalamu wa kimataifa huku akihamasisha vijana kuanza safari ya masomo yanayohusiana na TEHAMA.
“"Tangu tulipoanza shughuli nchini Tanzania mnamo 2007, Huawei Tanzania imejitolea kuhamisha maarifa na ustadi wa ICT kwa watanzania, na wataalamu wote kwa kuwajengea uwezo na utaalam wetu wa kimataifa na kuhamasisha vijana kuanza safari ya masomo yanayohusiana na TEHAMA. Tunafikiria kwamba nchini Tanzania, watendaji wataweza zaidi kubuni maarifa ya kina yahusuyo TEHAMA, na raia wa kawaida wataweza kuchunguza fursa na ustadi wa msingi kuhusu TEHAMA, na vijana ambao wanapenda masomo ya TEHAMA wataijenga nchi yao kwenye misingi ya dijitali."Alisema Zhang.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt Zainab Chaula (Katikati) akikabidhi Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Tecnolojia ya 5G kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Tanzania Dk.Samson Mwela (Kulia) wakati wa hafla fupi ya kutoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa na kampuni ya Huawei iliyofanyika Dodoma mwanzoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bwana Damon Zhang (Kushoto)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt Zainab Chaula (Katikati) akikabidhi Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Tecnolojia ya 5G kwa mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Anania Mashenene (Kulia) wakati wa hafla fupi ya kutoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa na kampuni ya Huawei iliyofanyika Dodoma mwanzoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bwana Damon Zhang (Kushoto).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment