KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Bashiru Ally amevunja mwiko kwa kuamua kummwagia sifa Rais Dk.John Magufuli kwa jinsi ambavyo amefanya kazi kubwa ya kupeleka maendeeo makubwa kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wa Mkoa wa Kagera.
Akizungumza leo mbele ya wananchi wa Komondo Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wakati wa mikutano ya kampeni ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Magufuli ambaye anaomba ridhaa ya kuongozewa tena miaka mitano mingine, Dk.Bashiru amesema Dk.Magufuli huwa hapendi kusifiwa lakini leo amevunja mwiko huo .
"Najua hupendi kusifiwa lakini navunja mwiko, kama utanitumbua basi unitumbue baada ya Uchaguzi Mkuu.Hapa ni kwangu,hapa nimeoa na nimefanya biashara hapa, nafurahi meli inafanya kazi wale ambao walifanya biashara ya ndizi wanasafirisha bila tatizo, nakusifu kwa jambo hilo.
"Watu ambao nimeponda nao kokoto wananijua, nilioendesha nao magari wapo hapa, Umenitoa jalalani lakini siri ya kunitoa jalalani ni elimu. Mwalimu Nyerere alisema ukitaka kumsaidia masikini usimpe pesa msomeshee mtoto wake, wewe umelifanya hilo,"amesema Dk.Bashiru.
Amefafanua shule zimekarabatiwa Bukoba kama ambavyo zimekarabitiwa maeneo mengine nchini nzima pamoja na kufanya maendeleo katika nyanja mbalimbali na ametumia nafasi hiyo kumshukuru kwa msimamo wake wa kujali wanyonge.
"Hii si sifa yako ya urais ni sifa ya kudumu ambayo inatokana na kazi uliyofanya.Nimekutana na Mwalimu uliyefanya naye kazi anasema alipokuona Sengerema ndivyo ulivyo.Umeanza kuonesha thamani ya uongozi na mzigo wa uongozi sidhani kama kuna mtu atatamani kuwa Rais kwa namna unavyofanya kazi.
"Ukweli msimamo wako ni wa kiwango cha hali ya juu sana.Ni kazi ngumu ya mateso, mimi mwenyewe siitamani. Mji huu umebadilika sana ,tukipata umeme wa kutosha na maji ya kutosha na kiwanja cha ndege ulichokijenga na meli unazojenga Kemondo hii itabadilika zaidi,"amesema Dk.Bashiru.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment