KILICHOSABABISHA SHIGONGO KUPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE,TIZEBA KUKATWA HADHARANI | Tarimo Blog


Na Said Mwishehe,MichuziTv-Buchosa

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli,ametoa sababu ya zilizosababisha kupitishwa kwa jina la Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa,Erick Shigongo badala ya Dkt.Charles Tizeba.

Dk.Magufuli ametoa sababu hizo za kukatwa kwa Tizeba katika mchakato wa kura za maoni wakati akihutubia Wananchi wa Buchosa.“Mchakato wa jimbo hilo ulikuwa wa kidemokrasia kura za Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Shigongo na Dkt.Tzeba zilifungana,”amesema Dk.Magufuli.

Amefafanua katika kuangalia walikuta Tizeba alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu hivyo alijipigia kura.Kwa mujibu wa taratibu za Chama jina lake likaondolewa na kupitishwa Shigongo ,hivyo ameomba wananchi kumpa kura nyingi yeye pamoja na mgombea huyo.

Wakati huo huo,Dkt.Magufuli amesema kuna mambo mengi waliyohaidi yakiwemo kuleta mapinduzi ya kweli kwa sababu nchi imetoka mbali.
Dkt Magufuli amesema umasikini unapoutamka kwenye ulimi ni kweli unaweza kuendelea kuwepo.

Amesema Tanzania ni tajiri ni lazima ianze kujitengemea yenyewe katika kuleta mabadiliko makubwa ya taifa.“Watanzania wenzangu tumeyafanya mengi,hata hapa Nyehunge hapakuwepo na nyaya za umeme lakini vijiji vingi tayari tumevipelekea umeme,”amesema.

Hata hivyo Dkt.Magufuli amesema nchi ya Tanzania sasa hivi inaonewa wivu kwani ilikuwa inahesabika kuwa ni nchi masikini na leo, iko uchumi wa kati.


 Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nyahunge katika Jimbo la Buchosa mkoani Mwanza katika mikutano ya Kampeni za CCM leo tarehe 8 Septemba, 2020.

 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2