Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi wa Tarafa ya Mkamba.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
Wananchi wakimsikiliza mgomea ubunge jimbo la Mkuranga.
Mwanachama mpya wakipokea Kadi za CCM
WANANCHI wa tarafa ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Mkuranga Pwani wameahidiwa kupatiwa gari ya kubebea wagonjwa katika kituo cha afya mkamba kilicho boreshwa ikiwa ni pamoja na kujaziwa vifaa, na kuletewa daktari wa upasuaji ili kuendelea kutoa huduma bora.
Aahadi hiyo imetolewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo Na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati alipofanya kampeni katika Kata ya Mkamba, Pupu na Panzuo zilizopo katika tarafa ya mkamba na kusema kituo cha afya Mkamba kilikuwa na halimbaya wakati anaingia madarakani lakini kwa juhudi za Daktari John Pombe Magufuli Sasa kimeboreshwa.
Ulega amesema ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kupitia ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 21/25 kila kituo cha afya nchini kitapatiwa gari kwa ajili ya kubebea wagonjwa.
Kwa upande mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mkuranga,Ally Msikamo aliposimama kuwaombea kura wagombea wachama cha mapinduzi akiwemo Rais, mbunge na diwani amesema
Hata hivyo Ulega amesema anaenda kuinua kiwango cha elimu mkamba kwa kujenga Shule ambapo ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Nyekenge, lengo nikuhakikisha Mkamba inapata wasomi wengi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment