LHRC YAWEKA MIKAKATI YA USAWA WA KIJINSIA. | Tarimo Blog


NA FARIDA SAIDY,MOROGORO

Katika kuhakikisha wanawake, watoto na watu wemyeulemavu, wanapata haki zao za msingi za kisheria kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu kimeendelea kutoa elimu kwa wadau wanaoshughurikia maswala ya makundi hayo,kwa lengo la kuweka misingi bora kati ya serikali na wananchi.

Akizungumza katika Warsha iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa wanaoshughurikia maswala ya wanawake,watoto na watu wenyeulemevu Mkoani Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na haki za Binaadamu BI Anna Henga , Amesema kuwa Moja ya Lengo ya Kituo Hicho Ni Kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha masuala ya Usawa wa Kijinsia yanazingatiwa katika jamii.

Aidha Bi Henga amesema semina hiyo inalengo la kujadili namna yakukabiliana na changamoto zinazowakumba wanawake,watoto na watu wenye ulemavu hususani waishio vijijini kwani wengi wao wamekuwa wakishindwa kutambua haki zao, wakati wakikutana na vitendo cha unyanyasaji.

Naye Mrakibu Mwandamizi kutoka Jeshi la Magereza SSP Amina Kavirondo amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu imesaidia baadhi ya mamlaka kufanya kazi kwa kufuata misingi ya Kazi hususani kutumia Sheria ipasavyo za kutetea na kulinda haki za watoto na wanawake.

Kwa Upande wake Hakimu Mkazi Mwandamizi kutoka Mahakama kuu Bi Rhoda Ngimilanga ameeleza kuwa katika Mahakama zote nchini kesi za watoto zinapewa kipaumbele katika kufanya Utekelezaji ulio thabiti kwa lengo la kupatikana kwa haki kwa muda muhafaka.

Licha ya hayo imeelezwa kuwa Mwaka 2019 kituo kimeweza kufanya Utafiti na kubaini haki za wanawake, Watoto na watu Wenye Uelemavu bado zinavunjwa kwa kiwango Kikubwa ikiwemo Ulinzi wao Dhidi ya Ukatili , kingono, na hata kupelekea mauaji.

Warsha hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbli wanaoshughurikia maswala ya wanawake,watoto na watu wenyeulemevu,wakiwemo Jeshi la Polisi,Mahakama pamoja na Jeshi la Magereza. 
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2