MAHERA :WANANCHI LINDENI AMANI,UTULIVU,PAMOJA NA KUFUATA UTARATIBU NA KANUNI ZA NCHI | Tarimo Blog

 Na Woinde Shizza, Vero Ignatius Michuzi TV Arusha



Zikiwa zimesalia siku 29 nchi ya Tanzania iingie kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 wa kumchagua Rais,wabunge na madiwani,wananchi wametakiwa kuilinda Amani,utulivu pamoja na kufuata taratibu na kanuni za nchi

Mkurugenzi Mkuu wa uchaguzi Dkt.Charles Mahera akizungumza na wadau wa Taasisi za kiraia,Viongozi wa dini ,wazee wa Kimila lna watu wenye mahitaji maalum alisema Tume imejipanga kuwa na Uchaguzi wenye utulivu wa hali ya juu.

Dkt Mahera alisema kuwa Kati ya wapiga kura 29,188,347 walioandikishwa wanawake ni 14,496,604 ambao ni sawa na 49.67%,vijana wenye umri wa Miaka 18-35 ni 15,650,998 Vijana wa kiume Ni 7,804,845 na wa kike Ni 7,846,153 

Aidha kuna jumla ya watu wenye ulemavu 13,211na Kati yao 2,223 Wana ulemavu wa macho ,4,911 Wana ulemavu wa mikono,6,077 Wana ulemavu wa aina nyingine

Alibainisha kuwa tume hiyo itatumia vituo vya kupigia kura 80,155 katika zoezi la kupiga kura tarehe 28/9/2020 ,Kati ya vituo hivyo Tanzania Bara itakuwa na vituo 79,670 na Tanzania Zanzibar itakuwa na vituo 685 pia itatumia vituo 1,412 vya NEC kwa upande wa Zanzibar tume imeridhia mipaka ya majimbo Kama ilivyorekebishwa na tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kila kituo Kati ya hivyo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500

Aidha aliwataka wadau hao kwenda kutoa Elimu kwa jamii na kuwaasa kwenda kumsikiliza Sera ili waweze kumchagua kiongozi wanaompenda 

Akichangia Mara katika kikao Askofu wa Kanisa la Menonite Amos Mhagachi alisema kuwa Ni vyema take makundi yanayifanya fujo katika kipindi Cha Kampeni wachukuliwe hatua za kisheria ili Amani iliyopo uendelee kutunzwa.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2