
SHIRIKA la hifadhi za Taifa (TANAPA) limewakamata raia 28 wanchini Ethiopia washukiwa kuwa wahamiaji haramu wakamatwa Usiku wa kuamkia leo Septemba 26, 2020 na Askari wa hifadhi ya taifa ya Saadani.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Kamishna Msaidizi mwandamizi-Mawasiliano, Pascal Shelutete imesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika eneo la Bahari jilani na Kijiji cha Buyuni.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa washtukiwa hao wamekabidhiwa kwa jeshi la Polisi kwaajili ya hatua za kisheria.
Hata hivyo taarifa hiyo inaeleza kuwa uongozi wa hifadhi hiyo umetoa onyo kwa wale wote wenye dhamira ya kutumia hifadhi za Taifa kuwa maeneo ya kufanyia vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria.
Lakini imeongeza kuwa wasithubutu kufanya hivyo kwani uongozi umejipanga vyema.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment