MKOA WA PWANI WATAKIWA KUJADILIANA PATAKAPOJENGWA CHUO CHA UFUNDI VETA | Tarimo Blog



MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka mkoa wa pwani kukubaliana kwa Pamoja kutenga eneo Kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi veta. 

Hatua hiyo imekuja baada ya mgombea ubunge jimbo la mkuranga na naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdalah Ulega kusimama na kumuomba mgombea mwenza huyo kuwajengea chuo hicho ili vijana waweze kupata ujuzi. 

Akizungza na wananchi maeneo ya vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani baada ya kusimamisha msafara wakati akielekea ikwiriri samia amesema serikali hawezi kujenga chuo kila wilaya, bali wachague eneo moja kwa ajili ya pwani yote.

Aidha mama samia amemtaka mkuu wa mkoa wapwani Mhandisi Evarist Ndikilo kwa kushirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha wanalipanga vizuri jambo hilo kwa kuwashirikisha wadau wa viwanda kuchangia ujenzi huo na pale patakapo bakia serikali itatoa pesa kwa ajili ya umaliziaji. 

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega amesema mkuranga kuna viwanda vingi,vijana wengi wanategemea kupata ajira viwandani lakini hawana ujuzi wa kuosha na kubakia kuwa vibarua. 

Ulega amesema upatikani wa chuo hicho utasaidia vijana kupata utaalamu, na kuondokana na dhana ya kuwa vibarua,kupata ajira na kukiajiri hali itakayo punguza hali ngumu ya maisha Pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe magifuli za uchumi wa kati wa viwanda. 

Katika hatua nyingine ulega amemuahidi mama samia ya kwamba mkuranga Rais atapata kura zaidi ya asilimia 90 na kuwataka wanamkuranga kuchagua chama cha mapinduzi kwa ajili ya maendeleo. 

Mohamed Maundu ni mgombea udiwani kata ya vikindu akizungumza mbele ya mama samia amesema changamoto za vikindu anazijua na atazipambania. 

Aidha Maundu ameishukuru serikali kwa kuanzisha miradi mikubwa katika kata hiyo ikiwemo kituo cha afya vikindu na shule.

 Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kulia) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi wa kijiji cha Vikindu ambapo amewaomba wanamkuranga kuchagua chama cha mapinduzi kwa ajili ya maendeleo. leo Agosti 24, 2020 wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. 
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa kijiji cha Vikindu Wilaya ya Mkuranga alipokuwa njiani akielekea Mkuranga kwenye Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM leo Septemba 07,2020
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo(kulia)akiteta jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega leo Agosti 24, 2020 wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. 

Mke wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga koa wa Pwani ,Mariam Ulega akiwasalimia wananchi kijiji cha Vikindu Wilaya ya Mkuranga  leo Septemba 07,2020.



Semu ya wananchi wa kijiji cha Vikindu Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wakishangilia baada  kuwasiri  Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2