Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi, (kulia) akiungumza kuhusu kuimarisha umoja pamoja na upendo katika kazi ili bodi iweze kufanya kazi zake kiufanisi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa PSPTB katika ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa Baraza la wafanyakazi wa PSPTB Simon Macha na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE-PSPTB Shilla Mwandu .
Mwenyekiti wa TUGHE-PSPTB, Shilla Mwandu kizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Baraza la wafanyakazi wa PSPTB Simon Macha na kushoto ni Katibu wa TUGHE- PSPTB Mawazo Lugusha.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha kujadili changamoto pamoja na mipango itakayowezesha Bodi hiyo kufikia malengo wakati wa mkutano mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akiwa kwenye picha za pamoja na wajumbe wa balaza la wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) wakati wa mkutano wao.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment