*Dk.Magufuli aahidi kutekeleza yote yaliyoahidiwa na Mwalim Nyerere
*Ataja hatua kwa hatua maendeleo yaliyopatikana mkoa wa Mara
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mara
MAELFU ya wananchi wa Mkoa wa Mara wamejitokeza kwenye mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli ambaye ametumia mkutano huo kueleza katika utawala wake yote ambayo Baba wa Taifa alipanga kuyatimiza lazima yeye ayatimize tena kwa kasi kubwa.
Amesisitiza atahakikisha Mkoa wa Mara anauenzi kwa kupeleka maendeleo hasa kwa kuzingatia ndio Mkoa ambao baba wa Taifa hili la Tanzania Hayati Julius Nyererere amezaliwa.
Dk.Magufuli akiwa katika mkutano huo amesema katika kumuenzi Baba wa Taifa katika kipindi cha miaka mitano Serikali ya Awamu ya Tano imefanya maendeleo makubwa katika mkoa huo ikiwemo kutoa fedha Sh.bilioni 49 kwa ajili ya kujenga uwanja wa lami.
"Nataka siku moja awe anapanda na ndege hapa hapa, na tutaendelea kuendelea na ujenzi wa miumbinu kwa ajili ya huduma mbalimbali.Ndio maana katika mipango yetu ile barabara ambayo Profesa Sospeter Muhongo ameizungumzia ya kilometa 92 zitatengenezwa bila matatizo.
"Hata watu wa Bunda walijichanganga wenyewe, walijichanganya wenyewe.Katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu imeeleza mambo mengi ya mendeleo kuhusu Mkoa wa Mara .Hata hivyo katika hali ya ubinadamu unapelekaje baraabaa kwa watu wanaokutukana, mimi ni binadamu na nina moyo na damu, hata kama unachakula unapeleka kwa watoto wako. Hata kama unajitajidi lakini karoho cha binadamu kapo,"amesema Dk.Magufuli.
Akifafanua zaidi kuhusua maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Mara ambapo amesema yale ambayo yamepangwa kufanyika katika mkoa huo kwa ajili ya maendeleo hayawezi kuyashinda.Hata hivyo akizungumzia kuhusu jimbo la Rorya amesema kuna tatizo la ukabila.
"Rorya kuna tatizo la ukabila, kuna makabila mengi, tangu tupate uhuru miaka 15 kabila la wajaluo ndio wamekuwa wakipata ubunge na imekuwa hivyo kwa muda mrefu, safari hii tumeona mgombea ubunge wa kule asiwe Jaluo , tunataka kuondoa haya mambo ya ukabila Rorya,"amesema na kuongeza Mwalimu Nyerere alikuwa Mzanaki na mama Maria ni Msimbiti lakini waliwaunganisha Watanzania wote pamoja na kuwepo makabila 120.
Ametumia nafasi hiyo kuwaambia watu wa Mara kwamba anawapenda na anawaomba kura ili kuendeleza yale ambayo yameanza kufanywa katika mkoa huo."Tumejenga hospitali saba za Wilaya
"Ila nasikia zile fedha za Wilaya za Musoma zimechelewa kutumika Sh.milioni 200 zimerudishwa kutokana na kuchelewa kutumia.Nataka zile fedha katika bajeti ya mwaka huu zije tukakamilishe ile hospitali , tumejenga vituo vya afya nane, zahanati 28 miradi yote imegharimu Sh.bilioni 21.2
"Wanaotibiwa pale ni Watanzania wote licha ya fedha kutolewa na CCM, katika maendeleo hakuna Chama lakini lazima kiwepo Chama cha kuongoza.Mara tumejenga shule za sekondari 35 , tumejenga shule za msingi, nyumba za walimu 158, vyuo vya ualimu viwili vya Tarime na Bunda vimekarabatiwa,wakati nakuja kuweka jiwe la msingi niliona Shule ya Msingi Mwisenge aliyosoma baba.
"Shilingi bilioni 45.6 zimekuja Mara kwa ajili ya kutoa elimu bure,katika nchi zinazotoa elimu bure tanzania ni kati ya nchi chache sana zinazotoa elimu bure, hata ulaya wanalipa, lakini hapa tuliamua kutoa elimu bure, fedha zinazokusanywa tuliamua zitumike kusomesha watoto wetu, hivyo tuliona hizi bilioni 49 zienda Mara kusomesha watoto.
"Ndio maana nimekuja tena hapa Mara kuomba kura li niendelee kutoa elimu bure, wasije wakaja watu ambao wataondoa utaratibu wa elimu bure.Kuhusu maji kuna miradi 38 imetekelezwa kwa Sh.bilioni 68.4, na tayari miradi 17 imekamilika, miradi mingine inaendele.Huduma ya maji sasa imeongezeka kutoka asilimia 44.4 hadi asilimia 66.9 ndio maana nimekuja tena kuomba kura
"Kuhusu umeme Sh.bilioni 105.4 zimetumika katika kupeleka umeme vijijini na katika Mkoa huu vijiji 411 vimefikishiwa umeme kati ya vijiji 458,hivyo vimebakia vijiji 47.Vijiji vilivyobakia haviwezi kutushinda, tumeshameza ng’ombe wote hatutashindwa kumeza mkia.Tupeni miaka mitano tukafanye maajabu katika umeme.
"Hivi sasa tuna Bwawa la Nyerere na umeme wake utafika hata Mara. hatutashindwa vijiji 47 vilivyobakia.Shilingi bilioni 171.2 zimetumika katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, hata hivyo ili miradi hiyo ikamilike na kutekelezwa imeemelezwa kwenye Ilan, ndio maana wamekuja kuomba kura tena,"amesisitiza Dk.Magufuli.
Ametumia nafasi hiyo kuelezea kura mbalimbali zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ambavyo imegusa mkoa wa Mara katika maeneo mbalimbali.
Amesema Ilani hiyo inazungumzia usafiri wa meli katika ziwa Victoria na Musoma itanufaika na utekelezaji wa miradi hiyo ya kuboresha usafiri katika ziwa hilo na hivyo itawezesha wananchi wanaozunguka ziwa hilo kufanya shughuli zao za kimaendeleo na kuleta uchumi kwa urahisi zaidi kwa kutoka eneo moja hadi jingine.
Amesema hata katika utalii Ilani imefafanua vizuri na ndio maana amegusia ujenzi wa uwanja wa ndege katika Mkoa wa Mara ambao utatumika pia kuleta watalii na hivyo kuongeza mapato ya wana Mara."Ni mengi yamo kwenye mipango, ni vugumu kutaja yote katika mkutano huu, ni mengi yamefafanuliwa, hata suala la bima Tanzania tuko mbele sana na katika mipango ya baadae tunaka kutoa bima kwa watu wote,"amesema Dk.Magufuli.
Sehemu ya Wanachi waliokusanyika katika uwanja wa Mukendo Musoma mkoani Mara kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Musoma katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM zilizofanyika katika viwanja wa Mukendo mkoani Mara.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere ambaye alimuombea Kura katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM zilizofanyika katika viwanja wa Mukendo mkoani Mara.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Mukendo kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Musoma mkoani Mara.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment