NINA USONGO SANA NA AKINA MAMA, WATOTO, VIJANA NA MICHEZO -TARIMBA | Tarimo Blog

*Gwajima atangaza kiama Kawe
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MGOMBEA Wa kiti cha Ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) Abbas Gulam Tarimba ameeleza azma yake ya kuwatumikia wakazi wa Kinondoni mara tuu atakapochaguliwa kuwakilisha jimbo hilo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Akizungumza leo katika viwanja vya MwembeYanga Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Urais Ubunge na Udiwani, kampeni zilizozinduliwa na Makamu wa Rais na mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia CCM Samia Suluhu Hassan, Tarimba amesema kuwa ataweka vipaumbele kwa wanawake, watoto,vijana na michezo kwa kuhakikisha anakuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto zinazowakabili.

"Nina usongo sana na wanawake, Watoto, Vijana na Michezo, tushirikiane tutoe kura za kutosha kwa CCM, nimekaa kwenye klabu za mpira, nafahamu kuwa klabu za mpira zina changamoto ya fedha, natambua changamoto zinazowakumba vijana katika harakati za kujikwamua kiuchumi, wanawake na watoto pia nitahakikisha wanapata huduma muhimu ikiwemo afya..... nawahakikishia nikiingia kwa kushirikiana na Serikali ya CCM tutapata majibu" ameeleza Tarimba.

Aidha Tarimba amehaidi kutatatua changamoto mbalimbali katika makundi ya akina mama, watoto pamoja na vijana ili kila mwananchi afaidi matunda yanayotokana na jitihada za Serikali.

"Tushirikiane, tumpe kura za kutosha Rais Magufuli ili tuipeleke Tanzania mbele zaidi ya sasa" amesema.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa jimbo la Kawe Askofu. Josephat Gwajima amesema kuwa jimbo hilo lipo kwa wapinzani kwa miaka kumi na kueleza kuwa imetosha na jimbo hilo litarudi CCM.

"imetosha, mmenipa kazi moja tuu...jimbo litaturudi CCM..Rais na Makamu wa Rais nawahakikishia wanaochechemea nitashughulika nao.....chafya imepita puani ni mwendo wa chafya." amesema Gwajima.

Aidha Gwajima amehaidi ushirikiano uliotukuka kwa wakazi wa Kawe katika kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa na kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma muhimu zikiwemo afya, elimu na Miundombinu. 

Shamrashara za kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 zimeanza sera mbalimbali zimeendelea kunadiwa katika majukwaa mbalimbali, ni kazi kwa wananchi kujitokeza na kuchagua viongozi watakaowafaa kwa miaka mitano ifikapo Oktoba 28 mwaka huu.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2