RAIS MAGUFULI AMEFANIKIWA KUJENGA UMOJA WA KITAIFA, TUSIKUBALI WANASIASA WATUGAWE-DK.BASHIRU | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Kagera

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Bashiru Ally amesema Rais Dk.John Magufuli amefanikiwa kujenga umoja wa kitaifa na umoja huo ndio unaweza kulivusha Taifa la Tanzania lakini cha kushangaza kuna wapinzani kwenye karne ya 21 bado wanazungumzia kuwagawa Watanzania.


Dk.Bashiru amesema hayo jana Septemba 16 mwaka 2020 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wakati wa mkutano wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Joh Magufuli.

“Nimefarajika sana wananchi wa Kagera, mapokezi haya ni makubwa sana,  sina cha kuwalipa ila Mungu atawalipa.Neno kubwa ambalo nataka kusema leo ahsanteni, mmekipamba Chama chetu, mmenonesha mshikamano, mshikamano wa kitaifa wa wana Kagera ndio utatuvusha , mshikamano wa kitaifa wa Watanzania ndio utatuvusha.

“Wapo wanaongopa wakiingia Ikulu wakipata nchi watakuwa na majimbo maaana yake nini, kila jimbo lijenge reli yale, walipe ada watoto wao.wajenge viwanja vyao va ndege.Kwa karine hii ya 21 kuzungumzia kuigawa nchi kwa mfumo wa majimbo haiko sawa kabisa,”amesema Dk.Bashiru.

Ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina namna Rais Magufuli anavyounganisha Taifa la Tanzania na Afrika kwa ujumla.”Kazi unayofanya ya kuunganisha Taifa letu, tena unaunganisha Afrika, kizazi hiki sio cha kuzungumza majimbo kwa kuligawa Taifa.Tunayo reli ya Tazara inaunganisha Afrika, anaiunganisha Tanzania na dunia kwa kujenga viwanja vya ndege lakini wapinzani wanazungumzia nchi kuigawa kwa majimbo.

“Wengine kama hatukosoma kwa mkono wa Serikali tungepata wapi jeuri ya kusimama mbele ya umati huu. Mabarabara yakatwe yawe ya majimbo, shule zikatwe ziwe za majimbo.Kuna  watu wanahubiri kuigawa nchi yetu, Baba wa taifa alikataa nchi yetu kugawanywa na kuvamiwa , tuliikomboa Tanzania dhidi ua Idd Amini.

”Tuliikomboa Uganda na Afrika dhidi ya madikteta, halafu anakuja mwana siasa kuomba kura ili akagawe nchi kwa mfumo wa majimbo.Wana CCM kokote mlipo chomekeeni kusema ukweli, lazima hawa waambiwe ukwelii,”amesema Dk.Bashiru,

Wakati huo huo amesema leo hii amesimama alipozaliwa, alipokulia, aliposomea  na alipoolea.”Nasimama hapa mbele yenu kuomba kura za mgombea urais.”



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2