Na. Samwel Mtuwa - Geita.
Mapema asubuhi baada ya kufunguliwa Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania GST leo Septemba 22,2020 Rais wa Chama Cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania FEMATA Ndugu John Bina atembelea Banda la GST lililopo katika maonesho ya Tatu ya Tekinolojia na Uwekezaji yanayoendelea katika viwanja vya Uwekezaji eneo la Bomba mbili Geita Mjini.
John Bina alitembelea katika Banda la GST akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa FEMATA ndugu Lister Balegela pamoja mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Viwandani Ndugu Kassim Iddi Pazi na viongozi wengine wa FEMATA .
Wakiwa katika Banda la GST Rais wa FEMATA na wasaidizi wake walipata elimu juu ya njia na mbinu mbalimbali za Utafiti wa Madini na Miamba kutoka kwa wataalam wa GST.
Kwa upande wake Bina alishauri kuwa Elimu na ujuzi juu ya Utafiti wa Madini uwafikie wachimbaji wadogo wa Madini ili watafute , wachimbe na wachenjue kwa kufuata mbinu za kisasa kwa lengo la kuleta tija ya kiuchumi katika shughuli zao.
Pamoja na ugeni huo GST imepata fursa ya kushiriki semina na wadau mbalimbali kutoka sekta ya Madini na taasisi za fedha iliyojadili juu ya Mpango Maalum wa ushiriki na Ushirikishwaji wa Wazawa katika sekta ya Madini nchini (Local Content) pamoja na Mpango Mahususi unao onyesha jinsi Mgodi utakavyo hudumia Jamii inayozunguka Mgodi (CSR).
Katika semina hii ya siku mbili GST inawakilishwa na Kaimu Meneja Mipango na Masoko Priscuss Benard na Mjiolojia Mkuu Sudian Chilagwire.
Zifuatazo ni Picha mbalimbali zikimuonesha Rais wa FAMATA na wasaidizi wake wakiwa katika Banda la GST na wataalam wa GST wakiwa katika semina ya CSR na Local Content.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment