Mkuu wa Masoko wa SAMAPAY ya Mbwana Samatta, Emmanuel Kirenzi na Mtumiaji wa SAMAPAY Grace Kambaulaya wakionesha namna ya kupakua application ya SAMAPAY kwenye simu kwaajili ya manunuzi ya vitu katika maeneo mbalimbali.
Mkuu wa Mikakati wa SAMAPAY, Emmanuel Massawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua huduma yamalipo kwa njia ya kidijitali ya SAMAPAY.
Na Ripota wetu, Michuzi TV
NYOTA Wa mpira wa miguu, Bwana Samatta amezindua huduma ya malipo kwa njia ya Mtandao wa "SAMAPAY."
Akizungumza na Waandishi wa Habari, kwa njia ya video mwanasoka huyo amebainisha kuwa mteja anayetumia huduma hiyo anaweza kujipatia punguzo la asilimia 5 kutoka kwa muuzaji anayetumia huduma ya SAMA Merchant.
“Mfano Pizza inauzwa Sh 10,000 mteja anayetumia SAMAPAY akifanya malipo kwa kutumia mfumo huu atapata punguzo la asilimia tano hivyo atalazimika kulipa Sh 9,500 na Sh 500 inayobakia ambayo kwa sasa inakuwa ndiyo pointi yenyewe anawekewa mteja.”Amesema Samatta kwa njia ya video
Hata hivyo samatta Amefafanua kuwa pointi hizo 5 zinazoingizwa kwenye SAMAPAY ya mteja kutoka kwa muuzaji zitamwezesha mteja kupata huduma nyingine ambayo thamani yake inalingana na wingi wa pointi atakazokuwa amekusanya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo katika ukumbi wa mikutatano wa Hoteli ya Hyatty Regency leo msemaji wa Mbwana Samatta, Alex Emmanuel amesema kuwa, SAMAPAY ni mtandao wa kidigitali unaomwezesha mteja kukusanya pointi ambazo zitamwezesha kufanya manunuzi katika migahawa, maduka au kupata huduma katika saluni hapa nchini kwa punguzo la bei kwa asilimia tofauti, kwenye maeneo ambayo yanapokea malipo kwa njia ya SAMAPAY.
Amesema kuwa ili kunufaika na huduma hiyo mteja anatakiwa kupakua duka mtandaoni(App) ya SAMAPAY kupitia Google Play Store huku wafanyabiashara kwa maana ya wauzaji wa bidhaa iwe migahawa, maduka au huduma nyingine yoyote wanatakiwa kupakua SAMAPAY Merchant.
"Mteja mwenye SAMAPAY akienda kununua bidhaa kwa wauzaji hao atanunua bidhaa kwa punguzo la asilimia kulingana na makubaliano na muuzaji husika, ambapo wapo wauzaji ambao wanatoa punguzo la asilimia 5 wengine 10 na kuendelea, hivyo muuzaji atamwekea mteja asilimia husika kama pointi katika SAMAPAY yake, hayo yatafanyika kwa ku scan QR ya mteja moja kwa moja." Amesema Emmanuel.
Amesema kuwa SAMAPAY imeasisiwa na kijana mtanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Uingereza katika timu ya Aston Villa, Mbwana Samatta kwa ushirikiano na kampuni kutoka nchini Korea, Paymaker kwa lengo likiwa kuwawezesha wananchi kunufaika malipo kwa kila bidhaa wanayonunua.
Amesema kuwa mteja akizikusanya nyingi zaidi anaweza kuzitumia kuchukulia bidhaa nyingine zenye thamani sawa na wingi wa pointi atakazokuwa amekusanya.” amesema Emmanuel
Kwa upande wa Mkuu wa Mikakati wa SAMAPAY ambaye pia ni Mkuu wa Utawala wa Mradi wa Samagoal wa mchezaji huyo, Emmanuel Massawe alibainisha kuwa “SAMAPAY ni app ambayo timu nzima ina jivunia malengo yake na manufaa kwa wananchi kwenye biashara, inaleta urahisi na unafuu kwa wateja nchini kwenye manunuzi” Amesema Massawe
Pia Mkuu wa Maendeleo ya Biashara, Mike Raymond amesema “ ni furaha kubwa kuwa sehemu ya mradi huo kwa kuwa umekuja kuleta mabadiliko nchini aliongeza kuwa baadaye mteja ataweza kufanya malipo moja kwa moja kutoka katika SAMAPAY”
Maeneo yanayotoa huduma kwa kutumia SAMAPAY ni Regency Park Hotel, Menbase, The rub spa, Terrace Lounge & Restaurant, Atsoko, Scott’s pizza na Mimi beauty salon na kupitia App hiyo wafanyabiashara watanufaika kwa kutangaza biashara zao, kuongeza mauzo, kuwasiliana kwa ukaribu zaidi na wateja ili nao kuzizoea bidhaa za mfanyabiashara husika pamoja na kujenga ukaribu zaidi na wateja.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment