SAU YAHAIDI KUJENGA MAKAZI BORA TANDALE NA MANZESE | Tarimo Blog


Mgombea wa kiti cha Urais kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU) Muttamwega bhatt Mgaywa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Tegeta kwa Ndevu, Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, na kuahidi elimu bure kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu pamoja na mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali, Leo jijini Dar es Salaam

Katibu mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) na mgombea wa kiti cha Ubunge jimbo la Kibaha Majaliwa Kyara akizungumza wakati wa kampeni za Chama hicho katika viwanja vya Sifa, Tandale jijini Dar es Salaam na kuahidi kujenga makazi bora zaidi kwa wakazi wa Tandale na Manzese, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sera Taifa kutoka SAU, Na mgombea wa kiti cha Ubunge jimbo la Kibamba Kunje Ngombale Mwiru akinadi sera katika viwanja vya Sifa, Tandale na kuahidi neema kwa wakazi wa maeneo hayo pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma muhimu, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti na mlezi wa Chama cha SAU Bertha Nkango Mpata akizungumza na wakazi wa Tandale na Manzese waliojitokeza kusikiliza sera zilizonadiwa na Chama hicho katika viwanja vya Sifa, Tandale. SAU imeahidi kuboresha makazi ya wananchi hao ikiwa wakiwapa ridhaa kupitia uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, leo jijini Dar es Salaam.
Kampeni zikiendelea



Burudani zikiendelea.




Mgombea wa kiti cha Ubunge katika jimbo la Kawe Maria Kakili akizungumza na wakazi wa Tandale na Manzese wakati wa kampeni za chama hicho, leo jijini Dar es Salaam.

wagombea wa nafasi mbalimbali wa Chama cha SAU wakiburudika mara baada ya kufungua kampeni katika viwanja vya Sifa, Tandale jijini Dar es Salaam.

Mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama cha SAU, akiwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, kushoto ni mgombea mweza wa kiti cha Urais Satia Mussa Bebwa, leo jijini Dar es Salaam.

Kampeni zikiendelea.

Mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya SAU, Akiendelea kunadi Sera katika viwanja vya Tegeta kwa Ndevu, wilaya ya Kinondoni.


Wananchi wakimsikiliza mgombea.


Mkutano ukiendelea.


* Ahaidi kutoa mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali na kuongeza ndege zaidi.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MGOMBEA URAIS kupitia tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU) Muttamwega Bhatt Mgaywa amehaidi kujenga makazi bora kwa wananchi wa Tandale na Manzese jijini Dar es Salaam kwa gharama za Serikali na kueleza kuwa maeneo hayo yamesahaulika miaka yote ukilinganisha na maeneo mengine ambayo yameendelea, yamekua na kufikiwa na huduma muhimu ikiwemo afya, maji na elimu.

Akizungumza leo katika mwendelezo wa kampeni zilizofanyika katika viwanja vya Sifa, Tandale jijini Dar es Salaam Mgaywa amesema kuwa ameishi katika maeneo hayo  kwa muda mrefu bila kuona yakibadilika, na kueleza kuwa wakati wa kubadilika ni sasa" amesema.

Mgaywa amesema, amedhamiria na wanahaidi pindi watakapoingia Ikulu watahakikisha maeneo ya Tandale na Manzese yanafanana na maeneo ya hadhi ya juu.

"Nimeona watoto wetu mnacheza ila matumaini hamna, maeneo ya Tandale na Manzese nyumba moja ina watu 50, chumba kimoja wanaishi watu 15 ni lazima maisha yetu yaendane na uchumi wetu" ameeleza.

Amesema kuwa akichaguliwa atakuwa na baraza la mawaziri kumi na wawili pekee ili kubana matumizi na fedha zitaelekezwa katika miradi ya maendeleo itakayowanufaisha wananchi.

Aidha amesema, Tanzania ni nchi tajiri inayoweza kusimama imara na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.
"Wajasiriamali tunafahamu changamoto mnazokumbana nazo, tutatoa mkopo wa shilingi milioni moja bila riba kwa wajasiriamali tiketi ya kuupata ni kitambulisho cha utaifa na tutaviboresha vitambulisho vya wajasiriamali vya JPM kwa kuweka picha" amesema.

Mugaywa amehaidi kuongeza ndege zaidi ili kuleta watalii wengi zaidi pamoja na kusafirisha bidhaa.

" Niliingia Bungeni kwa mara ya kwanza na Magufuli mwaka 1995, wakati wa kuapishwa nilipanda ndege na Magufuli na tulikuwa na ndege 7 za ATCL, sasa zimeongezeka na ninaahidi tutaongeza nyingine zilete watalii zaidi na kusafirisha bidhaa.... Rais ameonesha mfano tutasonga mbele zaidi" ameeleza Mugaywa.

Kwa upande wake mgombea mwenza wa kiti cha urais Satia Bebwa amewaahidi akina mama kutatua changamoto za afya kwa kuhakikisha wanapata huduma hizo bure.

"Nafahamu changamoto za akina mama hata vijana, elimu itatolewa bure hadi chuo kikuu na watoto kuanzia mwaka mmoja hadi miaka 18 watalipwa mishahara...tunazingatia usawa kwa wote na kuishi maisha yanayoendana na uchumi wetu" amesema.

Wakiwa katika Kata ya Kigogo SAU, wamefungua tawi la chama hicho na kupokea wanachama 52, ambapo pia wamehaidi huduma ya maji safi, elimu bure hadi chuo kikuu na uboreshaji wa miundombinu.

Pia katika Kata ya Tegeta, Wilaya ya Kinondoni SAU imehaidi kutekeleza ahadi zote ikiwemo mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali, elimu bure hadi chuo kikuu kwa utendaji uliotukuka kwa watanzania wote.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2