Wafanyakazi wa shule ya Sekondari ya St. Mark's wakiwa katika mahafali ya kidato cha nne.
Utambulisho wa wanafunzi kutoka shule zinazo milikiwa na MHL wakiwa katika Mahafali ya Kidato cha nne katika shule ya sekondari ya St. Mark's.
Utambulisho wa wanafunzi kutoka shule zinazo milikiwa na MHL wakiwa katika Mahafali ya Kidato cha nne katika shule ya sekondari ya St. Mark's.
Wahitimu wa Kidato cha nne wakiburudika na Muziki.
Wahitimu wa Kidato cha nne 2020.
Viongozi wa shule mbalimbali wakitoa vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo mbalimbali katika Mahafali ya kidato cha nne 2020.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
SHULE ya Sekondari Mtakativu (St.) Mark's mbioni kuanzisha kituo cha Kulelea watoto mchana (Day Care) watoto wa kuanzia miezi 9 hadi miaka miwili na nusu (2½).
Hayo ameyasema Mkuu wa shule ya St. Mark's, Leticia Kaijage wakati akizungumza na wanafunzi na wazazi jijini Dar es Salaam leo katika mahafali ya kidato cha nne ya 17 tangu kuanzishwa shule ya sekondari ya St. Mark's ambayo ni ya bweni na kutwa.
Amesema kuwa Shule ya St. Mark's imeshaanza mchakato wa kuwa na manesi wa kuwapokea watoto wadogo kwaajili ya kuwapima uzito na kuwaanda watoto kukua kimwili na kiakili kwani wazazi wengi wanajishughulisha na majukumu ya kutafuta kipato, lazima watoto wakae sehemu wenye uangalizi wa karibu kwa upendo na kwa amani.
Hata hivyo Mwalimu Leticia amesema kuwa katika kuhakikisha watoto wanakuwa vizuri wakiwa katika kituo hicho watahakikisha watoto wanapata mlo kamili wawapo kituoni na baada ya muda kuisha watoto watapelekwa nyumbani kwao kwa usafiri wa kituo hicho.
Akiwahusia wanafunzi wanaohitimu masomo yao katika shule ya St. Mark's, amesema kuwa elimu walio ipata ni bora waende wakaitumie vizuri kwa manuufaa yao na taifa kwa ujumla.
"Elimu mlioipata hapa St. Mark's ni elimu bora nendeni mkaitumie kwamanufaa yenu na taifa kwa ujumla." Amesema Mwalimu Leticia.
Jiepusheni na makundi yasiyofaa yanayoweza kuharibu nidhamu na tabia njema mlizozipata hapa St. Mark's, mkawe wasikivu kwa wazazi walezi na jamii kwa ujumla." Amesema Mwalimu Leticia.
Hata hivyo amewasihii kujiepusha na kujiadhari na magonjwa hasa UKIMWI ili isiwe sababu ya kutokuwa mfano kwa familia na jamii kwa ujumla na kutokuendelea masomo ya elimu ya juu.
"Kwa kipindi hiki ninawatakia maandalizi mema ya mtihani wa taifa mmtangulize Mungu katika maandalizi hayo na sherehe hii isiwaondoe katika uwanafunzi. Amesema Mwalimu Leticia.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Mtembei Holding Limited (MHL), Peter Mtembei amesema kuwa licha ya kutoa huduma ya elimu katika shule ya Sekondari ya St. Mark's, shule hiyo hutoa huduma ya maji bure kwa wananchi wanaozungukwa na shule hiyo.
Amesema kuwa kwa wazazi wanaosomesha watoto katika shule ya St. Mark's wanapata baraka zaidi kwani ada wanazo toa zinasaidia na jamii inayozunguka shule hiyo.
"Sadaka ambayo mmetoa wazazi na walezi katika shule hii ambayo ni ada, leo imewawezesha akinamama na watoto ambao walikuwa wanatafuta maji kwa umbali mrefu, sasa wanapata maji safi na salama hapa bila gharama yeyote, naamini yule mzazi aliyekuwa akihangaika kutafuta maji akiomba kwa Mungu kwa uwepo wa maji jirani baraka zinakuja kwako mzazi au mlezi mara mbili." Amesema Mtembei
Amesema kuwa kwa sasa ni miaka 20 tangu shule zinazomilikiwa na MHL kuendelea kutoa huduma ya Elimu katika jamii ambapo shule hizo ni shule ya Sekondari Ujenzi iliyopo wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, shule ya Sekondari na shule ya Msingi St. Methew, na Shule ya Sekondari ya St. Mark's iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na Shule ya Msingi iliyopo Iringa.
"Kuelekea miaka 20 ijayo tumejipanga kuboresha na kusimamia mambo makuu matatu ambayo ni kuhakikisha elimu inakuwa bora na kuanzisha darasa la Video na sauti (Audio Visual Classs), Kuwa na malezi mazuri pamoja na kuwa na usalama wa mtoto awapo shuleni na nyumbani." Amesema Mtembei.
Mahafali ya 17 ya kidato cha nne katika shule ya St. Mark's ilikuwa na wanafunzi 76 wasichana wakiwa 37 na wavulana 38 na kabla ya Kufanya sherehe za mahafali wanafunzi walionesha masomo kwa vitendo kwa wageni waalikwa na wazazi waliohudhuria mahafali hayo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment