MAMLAKA YENYE DHAMANA YA GOJU RYU KARATE DO JUNDOKAN TANZANIA.
Uongozi wa Goju Ryu Karate Do Jundokan Tanzania, chini ya mwenyekiti wake sensei Yusuf Kimvuli na SHIBU CHO (mkuu wa tawi) la Tanzania Sensei Rumadha Fundi.
Wanapenda kutoa ufafanuzi juu ya mfumo na taratibu za mambo ya karate na maelekezo ya kimuingozo kidogo.
Wadau wa karate Tanzania kuna umuhimu wa kuelewa mifumo na taratibu za hizi karate tunazofanya au kuzishabikia.
Panapotokea mtu kutaka kutangaza mfumo wake wa sanaa ya karate anayoifanya ajitahidi sana kuangalia taratibu za AFFILIATION anayofuata, au aweke mfumo mzuri kwa yale aliyojitungia bila ya kuathiri mifumo mingine iliyopo.
Kumekuwa na kawaida ya baadhi ya watu kuchanganya mambo, wakati mwengine bila ya kufahamu au mtu anafahamu ila anabuni udanganyifu kwa nia ya kupotosha mambo.
Haiwezekani uwe unafanya karate ya mfumo fulani au unacheza Kung Fu alafu unajitangaza kwa kutumia nembo ya Judo au Akido.
Au upo na AFFILIATION fulani ya karate alafu unavaa gii yenye nembo ya AFFILIATION nyingine kabisa isiyohusika na ambayo huna mahusiano nayo.
Hili jambo lipo sana hata ukiangalia kwenye mtandao wa Facebook utaona mtu amepozi au kufanya mbinu za ki kung fu lakini amevaa Gii au uniform za mchezo wa karate!
Hii wakati mwengine inatoa taswira kuwa makarateka wa Tanzania tumechanganyikiwa.
Kwa kawaida mtu anapopenda anaweza kusoma sanaa za mapigano (martial arts) aina mbili au tatu na akazifahamu vizuri,
ila huwa ni jukumu la huyo mtu kuchunga mipaka ya kila sanaa anayoifanya na kuiwekea heshima na staha zake.
Hapa kwetu Tanzania tuna aina nyingi za affiliation na walimu wenye kufahamu vizuri hii mifumo ya Karate, hivyo mtu anapotaka kujifunza ajiunge na moja wapo wa hizi affiliation ili apate kusoma kwa usahihi na ukweli katika sanaa ya Karate.
Si busara kuanza kubuni buni vitu kwa njia ya kuchanganya na kuwafundisha wengine kwa kuwapoteza.
Mtu anashauriwa ajifunze kupitia walimu na shule(club) zilizopo na zinazotambulika.
Pia ipo kawaida ya watu wengine ambao wamesoma Karate kwa kiwango fulani kisha wanatumia mwanya uliopo wa baadhi ya wananchi kutokujua namna mambo yalivyo.
Hivyo udanganya Umma kwa kuzua kwa makusudi au kuzitangaza sanaa zao kwa kupitia Nembo, jina la mtu mashuhuri kwenye sanaa hii au viashiria vya Club au shule nyengine ya karate.
Hili jambo si sahihi.
Kama unaanzisha jambo lako litangaze hilo jambo kwa kutumia vyanzo vyako na si wizi wa Nembo za wengine au kutumia picha za watu wengine mashuhuri wasiohusika na sanaa yako kwa kujitangaza wewe mwenyewe kwa faida yako.
Hao watu mashuhuri ni tunu katika fani yetu ya Karate lakini si mahala pake kuzichezea hizo tunu kwa kuwapotosha watu kwa kujifanya hao watu au nembo zao ni marafiki na wewe.
Kila kitu kinapaswa kuwa mahala pake kwa nidhamu na heshima za mafunzo ya Karate.
Uongozi wa Okinawa Goju Ryu Karate Do Jundokan Tanzania unapenda kutoa ushirikiano kwa Masensei wote Tanzania kuweka sawa hivi vitu ili kuweza kupatikana kwa umoja na mshikamano ulio thabiti.
Vile vile uongozi wa Jundokan Tanzani, unatoa mastikitiko yake kwa baadhi ya Masensei, Masenpai na Makohai toka Tanzania ambao wanatafuta "AFFILLATION" kwa Masensei wa JUNDOKAN kupitia njia za mtandao kwa kuomba urafiki kwenye "FACEBOOK" kwa nia ya kutaka kuwa matawi ya OKINAWA GOJU RYU KARATE DO JUNDOKAN nchini Marekani na nchi za Ulaya. Maombi yao huyapeleka hususani toka kwa ma Sensei waliokuwa marafiki wa aliyekuwa SHIBU CHO (mkuu wa tawi) Goju Ryu Jundokan Tanzania wa mwanzo, marehemu Sensei Bomani na pia SHIBU CHO (mkuu wa tawi) wa Tanzania wa sasa hivi sensei Fundi Rumadha.
Masensei hao waliopo nje ya nchi wamebaini kwamba wapo wanafunzi au ma Sensei toka Tanzania, hawana utamburisho wala mafungumano na chama cha GOJU RYu KARATE DO JUNDOKAN popote pale Duniani, lakini wamekuwa wakiomba wawe chini ya uongozi wa Masensei hao wa nje! Uongozi unadhani hawafahamu kwamba upo utaratibu muhimu wa kupitia kwenye matawi husasani TAWI LA JUNDOKAN TANZANIA na sio rahisi kuwa na utamburisho au “AFFILIATION" ya aina kama hiyo endapo kuna tawi tayari nchini Tanzania. Kwa kawaida hakuna utamburisho wa matawi mawili kwenye nchi mmoja.
Huwa kuna tawi moja ambalo huwa ni makao makuu, na wengine watakuwa chini ya hilo tawi lililopo ndani ya nchi.
Uhakiki wa mitindo ya karate, kama vile DAN au RANK za Club hufanyika kupitia kwa MWAKILISHI WA JUNDOKAN SHIBU CHO wa GOJU RYU KARATE DO JUNDOKAN TANZANIA mwenye utamburisho unaotambulika na kuwa na idhini toka SO HONBU (makao makao makuu) Assato - Naha - Okinawa - Japan chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, SENSEI KANCHO YOSHIHIRO MIYAZATO mwenye mamlaka yote ya JUNDOKAN SO HONBU DOJO DUNIA nzima, akisaidiwa na wateule wake, yani MASHIBU CHO au wakuu wa matawi kwenye nchi tofauti DUNIANI.
Hivyo mtu au sensei yoyote wa Tanzania hana budi kuomba usajili wa “AFFILIATION" kupitia TAWI LA JUNDOKAN TANZANIA ndio njia pekee sahihi ya kuwa "AFFILIATION"
Kwenye mfumo wa Goju Ryu Karate Do Jundokan Duniani chini ya mkuu wa Goju Ryu Jundokan Duniani sensei Kancho Eiichi Miyazato.
Goju Ryu Jundokan.
Mfumo wa Jundokan ni kuwa wakishakuwa na SHIBU CHO (mkuu wa tawi) kwenye nchi flani au nchi iliyopakana na nchi aliyekuwepo SHIBU CHO, tuelewe kuwa mtu hatoweza kupata uwanachama mwengine kwa kuandika barua kwa mwalim (sensei) yoyote wa Jundokan kwengineko Duniani ilikupata uanachama, au kuungwa na association hiyo ya Jundokan, hadi Mtu huyo kwanza apitie kwa huyo SHIBU CHO (mkuu wa tawi) aliyopo nchi kwake au karibu na nchi yake.
Afrika kwa sasa Goju Ryu Jundokan, SHIBU CHO wapo nchi 3 tu South Africa(Sensei Govinda) , Angola( Sensei Flameno) na hapa kwetu Tanzania (Sensei Fundi Rumadha 5Dan).
Kwa ufupi wapo wadau nchini wanawasiliana na sensei wa Ulaya na Amerika labda kwa kutofahamu wanataka wawe chini yao hao Masensei, jambo ambalo alipo hivyo kimiongozo ya Jundokan So Honbu,
Kwa miongozo ya Jundokan So Honbu ukiwasiliana na SHIBU CHO mfano wa Angola au South Africa kwa sasa kama unataka kujiunga Goju Ryu Jundokan utarudishwa kwa SHIBU CHO wa nchini kwako au nchi iliyopo karibu na nchi yako.
Wapo wadau wa karate Tanzania wanamruka SHIBU CHO wa hapa Tanzania na wanajaribu kufanya mawasiliano na Wakuu wa nje, matokeo yake wanaambiwa warudi kwa SHIBU CHO sensei Rumadha Fundi kuwasiliana nae na vilevile hao sensei wa nje wanampa taarifa SHIBU Cho TANZANIA, Sensei Rumadha Fundi kuwa kuna mtu kutoka kwenye eneo lako anataka kuwa chini yangu, nami nimemwambia awasiliane na wewe.
Taarifa hii ni kwa wale wote wanaojihusisha au kufanya Karate kwa Mfumo wa asilia wa Okinawa Gojuryu Karate Do Jundokan, yenye makao makuu ( So Honbu) Assato - Naha - Okinawa - Japan. Na pia ni taarifa kwa Makarateka wengine wanaotaka kuwa kwenye msingi Mzuri wa mawasiliano na ukweli. Si lengo la taarifa hii kuleta faraka. Milango iko wazi kwa mwenye mapenzi na Gojuryu. "yule anayejua ukweli, ukweli ndio utakaomfanya awe huru".
Sensei, Senpai kama una DOJO lako na unataka kujiunga na Goju Ryu JUNDOKAN karibu sana wasiliana na KATIBU MKUU TANZANIA KARATE DO JUNDOKAN 0715272069 SENSEI WAHID GHAFOUR ©️ kwa maelezo Zaidi©️.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment