TAKUKURU MANYARA YAMSHIKILIA MWENYEKITI WA BARAZA LA ARDHI BABATI | Tarimo Blog


Na Mwandishi wetu, Babati 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, inamshikilia Mwenyekiti wa Baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Babati, Mahelele Mussa kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 500,000. 

Mussa anatuhumiwa kuomba na kupokea kiasi hicho cha rushwa kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007. 

Kaimu mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Isidory Kyando ameyasema hayo mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari Septemba 25 mwaka huu.

Kyando amesema awali walipokea taarifa kutoka kwa mlalamikaji (jina lihahifadhiwa) ambaye alishinda kesi yake katika moja ya mabaraza ya ardhi ya kata ya mkoa huo na shauri hilo kukatiwa rufaa katika baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Babati. 

Amesema ilidaiwa kuwa kesi hiyo ya rufaa imekuwepo mahakamani hapo tangu mwaka 2016 bila kutolewa uamuzi na mlalamikaji huyo alipokutana na Mwenyekiti huyo kuuliza kuhusu sababu za kuchelewa huko kwa uamuzi wa shauri hilo ambalo yeye ni shahidi alitakiwa kupeleka shilingi 500,000 ili aweze kupatiwa upendeleo katika uamuzi wa rufaa hiyo. 

"Kutokana na imani waliyonayo wananchi wengi wa Manyara kwa TAKUKURU, mwananchi huyo alitoa taarifa kwetu zilizosababisha kukamatwa kwa Mwenyekiti huyo kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa hiyo," amesema Kyando. 

Amesema Mwenyekiti huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani September 29 mwaka huu baada ya kukamilisha mambo machache ya kiuchunguzi yaliyo salia

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2