Tamasha la wasanii Arusha Festival Lafana Mkoani Arusha | Tarimo Blog


 Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kennan Kihongosi akiongea na Wana Arusha katika tamasha la muziki wa kizazi kipya, Arusha Festival.
 
Msanii wa Kizazi kipya Marioo akutumbuiza katika Tamasha la Arusha Festival.
 
 =====  =======  ========

Na Jane Edward, Arusha

Tamasha la muziki wa kizazi kipya lililo washirikisha wasanii ndani ya Mkoa wa Arusha na nje ya Mkoa wa Arusha, limekuwa la matumaini makubwa ya kuamsha Hari ya burudani ndani ya Arusha.

Akizungumza katika Tamasha hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha na kushirikisha wasanii zaidi ya 30 kutoka Arusha huku wasanii wakubwa wakipamba Tamasha hilo wakiwemo Beka Flover,Kala Jeremiah,Dogo Janja,Marioo.

Mheshimiwa Kennan Kihongosi, amesema kuwa Arusha ilikosa burudani kwa muda mrefu na sasa ni wakati wa kuwapa fursa wasanii kutoka Arusha kuonyesha burudani kwa wana Arusha baada ya Majukumu ya kila siku.

"Kwakweli tamasha hili la Arusha Festival limekuwa la mfano kwani leo wananchi wangu wameweza kupata burudani ya kutosha na huu ni mwanzo tu,watarajie mambo makubwa chini ya serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dr John Magufuli"Alisema Kennan

Aidha alisema kuwa kufanyika kwa tukio hili linawapa fursa wasanii wa Arusha kuonyesha vipaji vyao na kubadilishana uzoefu na wasanii wakubwa

Kwa upande wake msanii wa Kizazi kipya maarufu kama Dogo Janja amesema kuwa yeye kabla ya kuwa msanii mkubwa alianza kuimba kupitia matamasha kama hayo na amefarijika kuona wana Arusha wamejitokeza kwenye tamasha hilo kuunga Mkono wasanii wa Arusha

Ameongeza kuwa yeye ni msanii kutoka Arusha na ameona baadhi ya wasanii wa Arusha walikuwa hawapatani Lakini kupitia Tamasha hili wamekuwa wamoja na hii ni hatua nzuri,Huku akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kuanzisha Tamasha hilo ,Arusha Festival.

Kwa upande wao wasanii wa Arusha wamemuahidi ushirikiano Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na ofisi yake katika kutoa burudani ndani ya Arusha na viunga vyake.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2