TCRA YAIPIGA FAINI IHSAAN RADIO | Tarimo Blog


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Joseph Mapunda(katikati) akisoma hukumu ya Radio Ihsaan FM ya kukiuka maudhui ya utangazaji ambapo radio hiyo imepigwa sh.milioni Tano jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

 MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipiga faini ya sh.milioni Tano Ihsaan Redio FM kutokana na kukiuka maudhui ya utangazaji.

Kituo hicho cha Redio kinatakiwa kuomba radhi kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 28  na kipindi cha Al Jawaabul kikifika hawatakiwi kurusha matangazo ya aina yeyote zaidi ya kuomba radhi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Joseph Mapunda amesema Kituo hicho cha  Redio kinatakiwa kuwa na waandishi wenye taaluma hiyo pamoja na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wao.

Mapunda amesema kuwa wasiporidhika na hukumu hiyo wanaweza kukata rufaa katika Tume ya Ushindani (FCC).

Aidha amesema Kituo hicho kinatakiwa kufuata Sheria za maudhui ya Utangazaji.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2