*Awaambia wananchi wa Singida kuna mambo makubwa yamefanyika
*Asema bilioni 470.4 zimetumika kwa ajili ya maendeleo katika mkoa huo
Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Singida
MGOMBEA urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli amehutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Singida wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kuwa Rais huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwa kipindi cha miaka mitano jumla ya Sh.bilioni 470.4 zimetuka kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo.
Akizungumza leo Septemba 1,2020 Mjini Singida Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kueleza maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na kazi hiyo ya kuendelea kuleta maendeleo itafanyika tena na kuomb wananchi wa mkoa huo katka Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu wampige kura.
”Tangu tumeingia madarakani miaka mitano iliyopita tumefanya mambo makubwa ya maendeleo.Kwa Mkoa wa –Singida peke yake jumla ya Sh.bilioni 470.4 zimetumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo,”amesema Dk.Magufuli.
Ametumia nafasi hiyo kuelezea wananchi wa Mkoa wa Singida namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutoa elimu bure na iwapo watachaguliwa kuongoza nchi wataendelea na jukumu hilo huku akisisitiza kuwa wataendelea kuboresha sekta ya afya, elimu, ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji , kilimo na kuendelea kuimarisha uchumi.
Akielezea kuhusu elimu Dk.Magufuli amesisitiza idadi ya wanafunzi wa shule za msingi imeongezeka kutoka milioni moja hadi milioni 1.6 na kwa wanafunzi wa shule za sekondari nako wameongezeka na hiyo inatokana na jitihada zinazoendelea katika sekta hiyo.
Wakati katika sekta ya maji nako, juhudi za kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana na wananchi wa Mkoa wa Singida wanafahamu namna hali ya upatikanaji maji ulivyokuwa miaka mitano iliyopita na sasa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani na kuweka mkakati wa kuondoa changamoto ya uhaba wa maji.”Ndio maana nmekuja tena kuomba ridhaa tukamalizie kazi tuliyoanza.”
Kwa upnde wa umeme, Serikali imefanya kazi kubwa ya kupeleka umeme katika vijiji mbalimbali nchini na jumla ya Shilingi bilioni 95.3 zimetumika kufikisha umeme katika vijiji 232 vya Singida.
Amegusia upande wa barabara ambao umefanyika katika kipindi cha miaka mitano na kwa Singida barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami huku akielezea ujenzi barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya ambayo itaendelea kumaliziwa.
”Tumejenga madaraja makubwa, tumeweka taa za barabarani na kazi inaendelea.Sote tunafahamu hii barabara ya Singida zamani haikuwa hivi, ilikuwa mbaya na wananchi wanateseka lakini hivi sasa iko vizuri inapitika na tutaendelea kujenga .Tumekuja kuomba kura kwa nafasi ya Rais, Ubunge na madiwani tukafanye kazi tuliyoanza kuifanya,”amesema Dk.Magufuli.
Amewataka wananchi kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo na kubwa zaidi kuchagua viongozi wenye watu ambao watamtanguliza Mungu .”Chagueni viongozi ambao wataleta maendeleo na wenye uzalendo kwa nchi yao.Mchague viongozi ambao katika miaka ya mitano wataleta maendeleo na sio kuwa na miaka ya mateso.”
Ameeleza namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano ambavyo imesimama imara katika kuziba mianya ya ubadhirifu wa fedha za umma kwa kuwabana mafisadi.”Zamani nchi yetu ilikuwa shamba la bibi lakini leo hii tumeziba mianya yote ya upotevu wa fedha , tumewabana mafisadi.”
Wakati huo huo amezungumzia Watanzania ambavyo Mungu amewavusha katika janga la Corona na hiyo imetokana na maombi ambayo nchi yetu yaliyofanyika kwa siku tatu.Amesema Mungu yupo na mataifa mengine duniani kutambua uwepo wa Mungu na katika yeye hakuna kinachoshindkana.
Dk.Magufuli amefafanua yeye ni binadamu lakini aliwaomba Watanzania kumuomba Mungu na hatimaye akasikia maombi yetu.”Corona imeaua watu wengi sana na bado unaendelea kuitesa dunia lakini kwetu sisi Mungu ameifanya nchi yetu kuwa Special.Majirani zetu bado wanakabiliwa na janga la Corona lakini hapa nchini kwetu tunaendelea na shughuli zetu.”

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment