UJENZI WA BANDARI YA KISIJU KUINUA UCHUMI,KUTOA FURSA YA AJIRA KWA VIJANA | Tarimo Blog


IMEELEZWA kuwa ujenzi wa bandari ya kisiju utatoa fursa ya ajira kwa vijana na kuinua uchumi kwa Wanamkuranga na nchi kwa ujumla.


Akizungumza na wananchi wa vijiji tatu vya kata ya kisiju wakati wa kampeni Abdalah Ulega amesema lengo lake ni kuona bandari inafanya kazi ili vijana waondokane na umaskini na wapate ajira.


Amesema bandari hiyo ya kisiju ambayo imekufa kutokana na mikoko kuota na mchanga kujaa, ilikuwa inapokea mashua 12 kwa siku lakini sasa inapokea mashua moja,ni jambo linalomuumiza lakini anapambana liweze kufanikiwa.

Ulega amesema ustawi wa kisiju ni bandari na barabara hivyo amewataka wananchi kuchagua Chama Cha Mapinduzi ili kiweze kutatua changamoto zao.

Sanjari na hayo Ulega amesema mpaka sasa zahanati tano zimefunguliwa, tisa zimekamilika ikiwemo zahanati ya koma na ishirini na sita zipo katika hatua mbalimbali.

Aidha Ulega amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi kuondoa makundi baina yao na kuwa na umoja na mshikamano kuhakikisha wagombea wote wa chama cha mapinduzi kinashinda kwa kishindo.

Hata hivyo Ulega amefanya kampeni katika vijiji vitatu vya kisiju,ambavyo ni koma,kwale pamoja na kisiju pwani vilivyopo kata ya kisiju .

 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi wa kijiji Koma na Kwale kata ya Kisiju ambapo amewaomba wanachama wa chama cha mapinduzi kuondoa makundi baina yao na kuwa na umoja na mshikamano il kuhakikisha wagombea wote wa chama cha mapinduzi wanashinda kwa kishindo.leo Septemba 09,2020 wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.



Mke wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga koa wa Pwani ,Mariam Ulega(kulia) akiwasalimia wananchi kijiji Koma na Kwale kata ya Kisiju leo Septemba 09,2020






Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo(kusoto) akisisitiza jambo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2