MGOMBEA ubunge jimbo la mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega ameaahidi kuwatoa unyonge wananchi wa kata ya kisegese iliyopo tarafa ya mkamba wilayani mkuranga mkoani pwani kwa kuwaboreshea miundombinu ya barabara ili kata hiyo iweze kufikika Kwa urahisi.
Akizungumza leo Septemba 13,2020 wakati wa kampeni akiwa katika kata hiyo ulega ambaye pia ni naibu waziri wa mifugo na uvuvi amesema kwa miaka mitano wamefanya mambo mengi ikiwemo ufunguzi wa zahanati ya chamgoi nakuboresha baadhi ya barabara ikiwemo eneo la kiyembayemba ambalo lilikuwa halipitiki kipindi cha masika lkn sasa panapitika.
Amesema Mkamba ilikuwa kama kisiwa mvua zikinyesha gari hazifiki lakini sasa usafiri unafika hayo yote ni maendeleo ya miaka mitano kupitia uongozi wa daktari John pombe magufuli ya hapa kazi.
Aidha ulega ameongeza kuwa visegese hakukuwa na shule lakini tayari wameshaanzisha ujenzi , zahanati chamgoi tayari inafanya Kazi, na kusititiza kuwa umeme utafika mpaka kijiji cha kibugumo na vijiji vyote vilivyoanzishwa ambavyo havijapata umeme vitapata.
Aidha Ulega amesisitiza kuwa kupitia ilani ya chama cha mapinduzi watafungua barabara zote ikiwemo ile ya kibesa na kizapara.
Hata hivyo amewataka wakulima na wafugaji kuacha kugombana na kuendelea kudumisha amani na utulivu na kuwaomba Kinamama kibesa, chamgoi na vianzi kumpa kura na ameahidi kutowaacha na ata waunga mkono katika shughuli zao za maendeleo.
Akiwa kata ya kimanzichana ambapo aliendelea na kampeni Ulega amezindua kijiwe cha wajasiria mali na nakuzungumzia changamoto ya shule na kuahidi kuongeza shule kutokana na uhaba ambapo amewahakikishia wananchi wa kimanzichana magharibi zahanati yao Ambayo imekamilika kwa kiasi kikubwa itafunguliwa hivi karibuni ili wananchi waweze kupata huduma
" tuliahidi kujenga zahanati na tumetekeleza mpaka Sasa IPO hatua ya mwisho, na katika kipindi hiki cha uchaguzi tuna peleka umeme pale naomba anzisheni nyumba ya mganga " Alisema Ulega
Mpaka kufikia sasa ulega ameshafanya kampeni katika kata nane za jimbo hilo ikiwemo kata ya kisiju ambapo amefika mpaka kisiwa cha koma na kwale na kuomba wananchi kuendea kukiunga mkono chama cha mapinduzi ccm kwa kukipa kura nyingi ili kikamalizie pale palipobakia.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment