Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Tangasisi Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
KATIBU wa UWT mkoa wa Tanga Sophia Nkupe akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo
MUWANIA Udiwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Pongwe Mecha Goodluck Matile akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa mkutano huo |
Msanii wa mziki wa Bongofleva Mwandeya akitumbuiza wakati wa kampeni hizo |
Msanii Kasimu Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo
“Ndugu zangu wavuvi nitahakikisha mnapata dhana za kisasa lakini pia kuimarisha umoja wenu katika kata ya Tanga sisi na Jiji lote la Tanga muweze kupata mikopo isiyo na riba na kununua vifaa vya uvuvi vya kisasa”Alisema
Akizungumzia suala la fidia ya barabara Kata ya Tangasisi hadi Mwahako alisema tayari alikwisha kuongea na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Tanga (Tanroad) na tathimini inaendelea ikikamilika watu wote ambao wapo barabarani watapata malipo.
“Ndugu zangu ninatambua hapa Tanga sisi hadi Mwahako kuna suala la fidia ya Barabara suala hili tayari nimekwisha kuzungumza na Meneja wa Tanroad Mkoa wa Tanga tayati tathimini inaendelea ikikamilika watu wote mliopo barabarani mtapata malipo yenu”Alisema
Hivyo aliwaomba wamchague kwa sababu ya uchungu alionao wa kuionga Tanga iweze kusonga mbele huku akiwataka wampe kuwa nyingi za ndio kwa sababu amedhamiria kuibadilisha Tanga.
Awali akizungumza katika mkutano hyo Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga Sophia Nkupe aliwaomba wapiga kura kumchagua mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu kwa sababu amelelewa na jumuiya hiyo.
“Lakini pia Ummy Mwalimu ni tunu kubwa tulioipata na kiongozi jasiri mwenye mafanikio hivyo wananchi hatupaswi kufanya makosa kwa kuipoteza”Alisema
“Ndugu zangu Ummy Mwalimu ni tunu kubwa tuliopata hivyo wananchi na wana Tanga hatupaswi kufanya makosa wakati wa uchaguzi mkuu tumpeni kura nyingi za ndio aweze kuilipatisha Jiji letu kutokana na mipango mizuri aliyonayo “Alisema
Katibu huyo aliwaomba wananchi hao kuhakikisha wana mpa kura za kishindo Rais Dkt John Magufuli ,Ummy Mwalimu na Diwani ili waweze kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo kwao
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment