Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro-KIA, Christina Mwakatobe, amesema mpango wa kuitangazia Dunia kuwa Tanzania ni salama kuhusu tishio la Corona umesababisha kupata watalii wengi kuliko nchi nyingine Duniani.
Aidha, Kiwanja hicho cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro kimefanikiwa kusafirisha mizigo mingi zaidi ya kilo Laki Tano tangu maambukizi ya virusi vya Corona yaliyoripotiwa nchini, mapema mwaka huu, hali iliyosababisha kupunguza kwa idadi ya Ndege zinazotua katika kiwanja hicho kipindi Cha Corona.
Hali hiyo imeelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa KIA, Mwakatobe katika Mahojiano Maalumu na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM katika Kiwanja cha KIA, ili kuainisha mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli katika kiwanja hicho.
Aidha, Mwakatobe amesema Watalii wanaotua katika kiwanja hicho cha Kimataifa wanashangaa ni kwa namna gani serikali ya Tanzania ilivyofanikisha kudhibiti tishio la Corona ambalo lilitishia dunia kuanzia mwezi wa Tatu mwaka huu 2020.
"Watalii wengi wameisifia sana Tanzania kwa jitihadi ilizochukua kujabiliana na Corona ambapo sasa Ndege niyingi za abiria na mizingo zinatua kwa wingi katika kiwanja hicho cha Kia". Alisema Mwakatobe.
" Mwezi wa Tatu na wanne hali haikuwa nzuri sana licha ya juhudi tukizochukua hapa KIA, tunashukuru sana kwani watalii wakishuka hapa wanashangaa mno Tanzania ilivyo salama" alisema.
Aidha, Mwakatobe amesema kwa sasa Mashirika Makubwa ya Ndege Duniani yanatua mara tatu kwa wiki katika kiwanja hicho, lakini kwa kuanzia mwezi ujao wa Kumi mwaka huu 2020 Ndege zitakuwa zinatua mara nne kwa wiki zikiwemo zile zinazobeba Maua za shirika la Ndege la Ethiopia.
Amesema hadi sasa mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kiwanja hicho cha KIA ni pamoja na kulinda ajira za wafanyakazi ambazo zingepotea wakati wa janga la Corona kwa kuwa Rais Magufuli mwenye uthubutu aliteisha gaza dunia.
Pia wamefanikiwa kununua magari matatu ya Zimamoto, kuboresha jengo la Abiria, kuongeza eneo la kutua na kupaa Ndege na kuimarisha hali ya ulinzi na Usalama kwa kununua pia Rada Mpya ya kuongozea Ndege.
Aidha, amesema kwa sasa wanaendelea kufanya mazungumzo na baadhi ya Mashirika ya Ndege yaliyositisha safari zao kutokana na tishio la Corona ambapo mazungumzo yamefikia hatua nzuri.
Nao wafanyabiashara pamoja na wakulima wa mboga mboga na maua waliozungunza na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM wamesifu hatua ikiyochukuliwa na serikali kupitia kiwanja cha KIA, kwani waliingia hofu wa bidhaa na mazao yao kuingia katika tishio la kufa mitaji yao pamoja na kukosa kipato.
Aidha, wameishukuru pia Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira, kwa kuwa karibu bao na kuwapa matumaini kuwa ugonjwa Covid-19 utapita na wataendelea na Biashara pamoja na usafirishaji wa mazao yao ama kawaida licha ya tishio hilo.
"Ujasiri waliooneshwa na JPM kwa kweli ni wa kupongezwa kwani angeamua kusitisha masuala ya watalii kwa kweli hali ingekuwa mbaya, hivyo tunampaongeza sana na hii sio Mimi tu hata wazungu wanapongeza kila siku wanapofika hapa KIA" walisema wananchi.
Awali walikuwa na changamoto ya Mizigo kwenda nje ya nchi lakini walikuwa wanasafirisha kwa wiki tani 70 tu.
Aidha wananchi hao wameuomba Uongozi wa Kiwanja cha KIA kuendelea kikitangaza Kiwanja hicho Kimataifa ili kuvutia Ndege nyingi za Ulaya kutua katika kiwanja hicho.
Tayari Kiwanja cha KIA nimepata Tuzo zaidi ya Saba kutokana na ubora wake Afrika na Dunia kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma za ufundi katika kiwanja cha Kia, Maritin Kinyamagoha, akizungumzia jitihada zilizichukuliwa wakati wa Corona, amesema miezi kadhaa iliyopita baada ya anga kufunguliwa walifanya vikao na wadau wa viwanja wa Ndege kwa kufanya mafunzo kwa wafanyakazi ya namna ya kuwapokea wageni wanaotoka kwenye nchi zenye maambukizi ya Corona.
" Cha kwanza ilikuwa nikupokea cheti cha usalama wake pamoja na kujaza Fomu huku wakiwataka kuzivua barakoa kwani huenda zikawa pia na maambukizi ya virusi vya Corona" alisema
Waliweka matangazo sehemu mbalimbali kuhusu namna ya kujikinga na Corona katika Viwanja vya Ndege.
Kwa upande wake Lucas Gamage ambaye Ni mjumbe wa kamati ya Chama cha wasafirishaji na wamiliki wa Taxi, amesema Corona ilisababisha baadhi ya vijana kukosa ajira kwani vijana waliendelea kufanya kazi kwa kiwango Cha chini tofauti na awali ambapo hapakuwa na ugonjwa wa Corona.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment