UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA JIJINI MWANZA NDIO SABABU ZA KUJENGWA KWA UWANJA WA NDEGE CHATO | Tarimo Blog


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chato

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amesema Dk.John Magufuli katika Awamu hii ya Serikali ya Awamu ya Tano ndio amejenga viwanja vingi vya ndege, kupanuliwa, kuwekewa lami kuliko wakati mwingine wowote na viwanja vimejengwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Polepole amesema hayo leo Septemba 11,2020 akiwa Chato mkoani Geita wakati akizungumza na waandishi wa habari walioko kwenye kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli.

Amesema awamu hii mbali ya kujenga viwanja vya ndege pia imeendelea kufanya matengenezo kwa viwanja vya zamani kuhakikisha navyo vinakuwa katika kiwango kinachotakiwa."Mtwara, Tabora ilikuwa changarawe tupu, Kigoma, Shinyanga , Bukoba tayari imemalizika na jengo nalo tayari katika uwanja huo.Mikoa inawekewa viwanja vya ndege inakuwa nongwa, hii ni mbaya sana , wapinzani wako kama nywele inakatwa leo kesho inaota.

"Tulikuwa Singida mgombea wetu wa urais amesema anaweka uwanja wa ndege Singida , tukiweka pale tunamuwekea Mbowe?Mwalimu Nyerere alikuwa ameweka uwanja wa ndege katika mikoa na Rais Magufuli anakwenda kuuboresha ukiwemo ule wa Nachingwea. Geita ni mkoa mpya haukuwa na uwanja wa ndege.Imewekwa uwanja wa ndege tena hauko mjini.

"Kubwa kuliko, tumenunua ndege nyingi kwa ajili ya kuhudumia Watanzania wa mikoa yote, ndege hizo kwa ajili ya kuchukua watu mbalimbali na tumesema tutandaza viwanja vya ndege.Kwa hapa Geita mnafahamu Rais Magufuli ameifungua Mwanza katika dunia, uwanja wa ndege Mwanza ndio mrefu kuliko uwanja wowote ukanda huu, unakaribia kilometa nne.

"Kwa hiyo umepatiwa hadhi ya kimataifa, vigezo vya kidunia unapokuwa na uwanja wa kimataifa lazima uwe na uwanja mwingine wa kimkakati, unapopata shida ndege iweze kutua.Hakuna sababu ya kwenda Dar es Salaam ni ni mbali, Kimalanjaro nako ni mbali, na uwanja wa karibu ni Geita na kama Mkoa umepata uwanja wa ndege, ninaposikia mtu anasema kuhusu viwanja vya ndege inashangaza sana, "amesema Polepole.

Wakati huo huo amesema katika eneo ambalo Rais Magufuli amefanya ni kupandisha hadhi ukanda huo ambao unaziwa Victoria , ukiacha visiwa vya saa Nane, Rubondo na Burigi Chato kote huko ni mbuga za wanyama."Pori haliingizi fedha lakini unapofanya kuwa mbuga za wanyama watalii wanakuja na kuleta fedha ambazo zitakuwa zinakwenda kuleta maendeleo, kwa hiyo watu kama hawa ambao wamekuwa na tabia ya kupotosha wapuuzwe.

"Kwa hiyo nitoe rai Oktoba 28 mwaka huu, wewe unayependa maendeleo ya Tanzania , unayeona tunakwenda mahala fulani hakikisha kura yako inakwenda kwa mgombea wa CCM.Kuna maeneo mengi ambayo yalikuwa nyuma kimaendeleo, Ziwa Nyasa hakukuwa na meli hata moja, leo hii kuna meli tatu, Ziwa Tanganyika nako usafiri wa meli umeimarishwa.Ziwa Victoria huko ndio mambo makubwa yamefanyika haswaaa.

"Katika madini kuna kazi kubwa imefanyika, umepigwa ukuta kule kwenye madini ya Tanzanite.Hapo awali kwa mwaka ilikuwa zinachimwa kilo  300 za dhahabu kwa mwaka leo hii wazinapatikana zaidi ya kilo 6000 za dhahabu.Watoto wanakwenda shule bila malipo,

 "Halafu wanasema unafanya maendeleo ya vitu badala ya watu. Ukurasa wa 83 unazungumzia kuimarisha mfumo wa afya ya bima , huwezi kutoa bima ya afya wakati hakuna miundombinu au kwa lugha nyepesi unaweza kupanda mbegu wakati shamba hujaandaa.Oktoba
28 kura zote ni za kuchagua mafanikio, kazi iendelee, kura zote kwa Dk.John Magufuli na ndani ya miaka mitano Tanzania imekuwa kinara wa nchi ambayo inauchumi jumuishi , wanakuwa wakubwa na wadogo,"amesema .

 Amefafanua mwaka 2019/2020 Tanzania imeingia nchi zenye uchumi wa kati na hiyo maana yek ni kwamba nchi inazidi kuaminika zaidi, inakuwa na uwezo wa kukopa zaidi wakati katika Ilani za wapinzani wao wanasema  watafuta kodi."Yesu alisema ya Kaisari muachie Kaisari, hivi unaposema utafuta vitambulisho vya Machinga unataka kuwarudisha wapi, unataka wawanyanyasike , na  Watanzani muwe macho.

"Ukisoma Ilani ya Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa Chadema) wana mambo ya kutisha wanakwambia watakapoingia madarakani madini yote watatumia kuweka rehani,maana yake wanakwenda kukopa kwa kuweka dhamana isiyohamishika , watu malaghai, wanataka kuuza nchi yao.Nenda kwa kwa Zitto Kabwe (ACT Wazalendo),"amesema Polepole na kuongeza usione vyaelea vimeundwa tena kwa uchungu mkubwa.

Amesisitiza wapo watu hawawajibiki  Tanzania bali wanawajibika kwingne, ndio maana wanakwenda na kurudi lakini kwa Dk.John Magufuli anashinda hapa hapa, hata Afrika anakwenda kwa kudonoa, anamuacha Makumu wa Rais aende .yeye anabaki kusimamia maendeleo."Wanasema watabadili umiliki wa madini, hapa ndipo tunapigwa bao, kazi ambayo Rais Magufuli anaifanya sio kwamba watu wanapenda, sheria ya madini iko Tanzania tu.

"Tazama Ilani zao mtu anasema ataleta ubwabwa, mwingine anasema kazi na bata na bata ni starehe, hawa watu wanaongozwa na shetani. imeandikwa utafanya kazi kwa jasho lako, unachotakia ni kufanya kazi wa unyenyekevu.Mwingine anakuja na uhuru , haki na maendeleo , hivi hii ni kauli mbiu?Na siku ya kwanza wanakwenda wanatukana watu, anasema maji wetu hawajui Kingereza, amekuwa akituna watu kila siku.
Rais Dkt John Pombe Magufuli aliposhuka kwa mara ya kwanza Uwanja wa ndege wa Chato alipokwenda mapumzikoni nyumbani kwake hivi karibuni (Picha na Maktaba.)

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2