Imani Sichalwe Kaimu Msajili Bodi ya Nyama nchini Tanzania.
======= ======= ========
Na.Vero Ignatus
Wafanyabiashara wa Mazao yatokanayo na Mifugo wametakiwa kufuata Sheria na taratibu za uingizaji na ufanyaji biashara za bidhaa hizo ,kama inavyoelekezwa kwa Mujibu wa Sheria ya Maziwa namba 8 ya Mwaka 2004 na Sheria ya Nyama Namba 10 ya Mwaka 2006.
Akizungumzia Oparesheni hiyo maalumu ya ukaguzi wa Mazao yatokanayo na Mifugo Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Bwana Imani Sichalwe ambae pia ndie kiongozi wa Oparesheni hiyo maalumu Kanda ya kusini amesema,Imefika wakati wafanyabiashara wa Mazao yatokanayo na Mifugo Kuwa na Utamaduni wa Kufuata Sheria zilizopo ili Kulinda afya ya Mtumiaji ikiwa na kuendelea Kuongeza mapato ya Serikali.
Bwana Sichalwe amesema kuwa Oparesheni hiyo maalumu inahusisha Mikoa ya Mbeya na Songwe lakini itafanyika nchi nzima na ni Muunganiko Utekelezaji wa Majukumu kwa Pamoja Kati ya Bodi ya Maziwa Tanzania na Bodi ya Nyama Tanzania na Kuomba Wananchi watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa, zitakazowezesha kubaini wale wote wanaokiuka Sheria na Taratibu za Ufanyaji biashara wa mazao yatokanayo na Mifugo.
Aidha Mkuu huyo wa Oparesheni ameongeza kuwa katika Ukaguzi uliofanyika hivi Karibuni Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, wamebaini Uingizwaji wa Maziwa Kutoka Afrika kusini na Malawi kinyume na taratibu ,Pamoja na kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa nyama, wanaoendesha shughuli hiyo kinyume na Taratibu na Sheria zilizopo.
Bwana Sichalwe ametoa rai kwa Wafanyabiashara wote wa Mazao yatokanayo na Mifugo Kufuata Sheria na endapo yeyote atakae kamatwa akifanya biashara ya mazao yatokanayo na Mifugo Kinyume na utaratibu hatua Kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi ya Mtu huyo na Serikali ipo Macho Wakati Wote
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment