WAJASIRIAMALI WA BIASHARA NDOGO NDOGO WAPEWA MAFUNZO NA CHUO KIKUU MZUMBE JIJINI DAR | Tarimo Blog

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akizungumza na wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo katika semina ya siku tatu kuanzia Septemba 23 hadi Septemba 25,2020.
Baadhi ua wajasirimali wa biashara ndogo ndogo wakisikiliza mada katika mafunzo yanayoendelea kutolewa Chuo Kikuu Mzumbe Kamasi ya Dar es Salaam.

CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam,  wakishirikina na Kuehne Foundation wameandaa mafunzo ya biashara na usafirishaji na ugavi kwa wafanyabiashara ndogondogo (VIBINDO) wa jijini Dar es Salaam.

 Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika katika  Kampasi ya Dar es Saam  Kuanzia  leo Septemba 23 hadi Septemba 25, 2020.

Akizungumza na Michuzi Blog Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam na Mratibu wa Mradi wa Kuehne Foundatin, Dkt. Omary Swalehe amesema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo katika ugavi na usafirishaji wa biashara zao.

"Kwa kipindi cha kwanza katika mafunzo haya tumeweza kuwaeleza kinagaubaga jinsi Wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo namna ambavyo wanaweza kufaidika na usafirishaji na Ugavi katika kuboresha biashara zao." Amesema Dkt. Omary

Hata hivyo Dkt. Omary amesema kuwa kwa sasa ni zamu ya wafanyabiashara wa biashara ndogo ndogo ili kujua umhimu wa ugavi katika biashara zao.

Amesema kuwa mafunzo hayo yatawanufaisha wafanyabiashara wadogo wadogo ili kila mmoja atumie mafunzo hayo katika biashara zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akizungumza wakati akitoa mafunzo kwa wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo amesema kuwa kila mtu ananjozi za kuwa mjasiriamali lakini sio wote wanaofikia malengo yao.

Amesema ni lazima Mjasriamalj kumwambia mtu mwingine malengo yake ili anapotimiza au anapokaribia kutimiza au kushindwa kutimiza malengo mtu lazima ahoji kulikoni malengo hayatimii ili mtu aweze kuongeza juhudi katika malengo yake.

Na kwa Upande wa Mtoa mada, Dkt. Maulid Nzaganza amesema kuwa mafunzo hayo yanawasaidia wajasiriamali kuongeza thamani katika bidhaa ambazo zinathamani ndogo kwa kutumia Teknolojia rahisi.

Amasema teknolojia hiyo rahisi wajasiriamali hutumia mitandao ya kijamii katika kutangaza biashara zao na kuongeza thamani biashara hizo kwa ushindani mkubwa watu wanatumia teknolojia.

Dkt. Nzagaza amesema kuwa wajasiriamali wadogo wadogo wanaweza kutumia teknolojia kwa mtaji mdogo aliokuwa nao bila ya kuwa na mtaji mkubwa wa kukopa na wenye riba kwa kuuza bidhaa kubwa.

"Hapa nimewaonesha bidha iliyokuwa ikiuzwa bei ndogo na baada ya kutumia teknolojia rahisi bidhaa ile ile inaongezeka thamani." Amesema Nzaganza

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa wamepata elimu ya kutosha juu ya masoko ya biashara zao na si kufanya biashara bila malengo.

Mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa na Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam wakishirikiana na taasisi ya Kuehne ikiwa ni mafunzo yanayomalizia kipindi cha awali cha Mradi.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2