WAKAZI KIJIJI CHA LENDKINYA WILAYANI MONDULI WAISHUKURU SERIKALI KUWAPATIA UMEME | Tarimo Blog


Na Woinde Shizza,Michuzi Tv ARUSHA

WAKAZI wa Kijiji cha Lendkinya kilichopo wilayani Monduli mkoani Arusha wameishukuru Serikali ya Awamu ya tano kwa kuwapatia huduma ya umeme ambayo itawasaidia kuondokana adha ya mifugo yao kushambuliwa na wanyama wakali nyakati za usiku

Wameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa uwashaji wa umeme wa Rea Kijiji hapo uliofanywa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli Robert Syantemi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli  ambapo aliwataka wananchi hao kutumia umeme huo kwa faida.

"Tunaweza kutafuta utaratibu wa kujenga viwanda mbalimbali vikiwemo viwanda vya usindikaji wa maziwa pamoja na ngozi ,pia umeme huu utasaidia watoto wetu kuweza kujisomea hata katika kipindi Cha usiku,vyote hivi vikiwa ni fursa ya Maendeleo ambazo zinaweza kutumika na kupatikana kupitua huduma hii ya umeme"amebainisha Robert

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa umeme   nchini Innocent Luoga  alisema la ufungaji wa umeme katika Wilaya ya Monduli linaendelea vizuri na hadi sasa vijiji 35 vinaendelea kupatiwa umeme na vitawekwa umeme

Alibainisha katika vijiji hivyo vijiji sita vinaendelea kupatiwa umeme katika Mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza na vijiji vingine 29 vitawekwa katika mradi wa umeme wa REA mzunguko wa tatu awamu ya pili ambapo hadi ikifika Septemba mwaka 2021 vijiji vyote nchini vitakuwa na umeme

Alibainisha kuwa Tanzania inavijiji 12268 ambavyo vilikuwa vinatakiwa kuwekewa umeme na vijiji hivi vinatoka na takwimu za Tamisemi ambapo hadi sasa vijiji 9600 teari vimeshawekwa umeme na vijiji 2600 ndio vimebaki ambapo alifafanua hadi ifikapo 2021 vijijiji vyote vitakuwa vimewekwa umeme.

Kwa upande wake Meneja wa umeme mkoa wa Arusha  muhandisi  Herin Mhina  alisema kuwa umeme huu wamefunga kwa wiki mbili Kama vile waziri wa Nishati alivyoagiza kipindi alivyokuja kutembelea Mradi huo.

"Mkandarasi aliekuwepo hapa alimsimamisha kazi kutokana na kushindwa kumaliza kazi kwa wakati na kazi hii  tulikabithiwa Tanesco na tulipewa mda wa kufanya na tumetekeleza ninachotaka kuwaambia wananchi tujitahidi kulinda miundo mbinu hii ya umeme, "alisema Mhina.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli  Robert Syantemi akikata utepe ikiwa ni shara ya kuwasha umeme rasmi katika kituo cha afya cha Lendkinya kilichopo katika  kijiji Cha Lendkinya  wilayani Monduli ,mwishoni mwa wiki  wakati wa uwashaji wa umeme wa Rea katika Kijiji hicho ambapo wananchi zaidi ya 9000 watanufaika na umeme huo .(picha na Woinde Shizza ,ARUSHA).
 Ofisa Tarafa ya kisongo Paulo Kitereki akizungumza Wananchi wa  Kijiji cha Lendkinya wakati wa Zoezi la kuwasha umeme katika Kijiji hicho
 Meneja Umeme mkoa wa Arusha Herin Mhina akisoma taarifa fupi ya Mradi wa Rea Wilayani Monduli
Kamishna msaidizi wa umeme   nchini Innocent Luoga   akizungumza wakati wa uwashaji wa umeme katika Kijiji Cha Lendkinya kilichopo Wilaya Monduli .

  katibu tawala wa Wilaya ya Monduli Robert Syantemi akizungumza  na wananchi wa Kijiji Cha Lendkinya wakati wa uwashaji umeme katika kijiji hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya Robert Syantemi akimkabidhi mwandishi wa habari Amiri Mvungi kutoka ITV  kifaa aina ya Umeta kinachotumika kusambaza umeme Ndani ya jengo dogo la kuishi au la biashara ,vifaa vilivyotolewa Kama zawadi kwa waandishi wa habari na shirika la umeme TANESCO .Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa katika Kijiji Cha Lendkinya ,Ndani ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha (picha na Woinde Shizza ,Arusha

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2