MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kigamboni Kwa tiketi ya Chama cha Act-wazalendo Mwanaisha Mndeme amewaomba wananchi wa Kigamboni wamchague ili awe mbunge wa Jimbo hilo huku akihaidi kulinda haki za wavuvi Wilayani humo.
Amesema kuwa ni miaka zaidi ya kumi Sasa jimbo hilo limekuwa Chini ya chama cha Mapinduzi CCM lakini hadi leo vijana wakigamboni karibu asilimia 79 hawana ajira rasmi.
Mwanaisha ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya Tungi Mnadani Kigamboni jijini Dar es salaam ambapo amesema endapo wananchi wa Kigamboni wakimchagua hatua ya Kwanza nikushughulikia changamoto za wavuvi.
"Nina waomba ndugu zangu mnichague kwani shida zenu nazijua na ni za miaka mingi sekta ya uvuvi, ukosefu wa ajira Kwa vijana, mikopo Kwa akina mama, ukosefu wa huduma bora za Afya, haya yote mkinichagua nitakwenda kuyashughulikia."Amesema Mwanaisha
Ameongeza kuwa Kigamboni kunachangamoto ya makazi bora hivyo Kama watamchagua atatumia elimu yake ya uwanasheria na kushirikiana na watu wa mipango miji na mazingira kuhakikisha wanapima Ardhi ili wananchi wapate fursa ya kukopesheka.
Amesema kuwa miaka kumi ya mbunge aliyemaliza muda wake ni miaka ya changamoto nyingi Kwa wananchi wa Kigamboni na ndio maana hata yeye mwenyewe anakiri huku aliwataka ninyi wananchi mumchague tena ili akamalizie kazi .nakwamba wamkatae kwani hatoshi.
"Ndugu zangu mimi ni biti mdogo lakini ni mwanasheria nawahakikishia mkinipa kura nakwenda kufanya mambo makubwa Kwa ajili ya Kigamboni yetu si mnajua changamoto za afya zilivyo dawa tatizo, lakini upande wa elimu madarasa machache katika shule zetu nitahakikisha mkinichagua tunakwenda kumaliza kero hii." Amesema Mwanaisha
Amefafanua kuwa katika halmashauri kuna mikopo asilimia kumi inayotoka katika makundi matatu tofauti ambayo ni vijana, akinamama na walemavu
wakimchagua atakwenda kuwapigania ili wanufaika wote wapate kwa usawa.
Pia amezungumzia kuhusu soko la wilaya ya Kigamboni amesema kuwa kwa muda mrefu limekosa soko la uhakika hali inayowalazimu wananchi kufuata huduma nje ya Kigamboni wakati maeneo ya wazi yapo wakimchangua atashughulikia changamoto hiyo ambayo inawakabili.
Alimaliza Kwa kuwaomba wananchi hao ili mambo yaende vizuri basi wahakikishe wanampa kura Diwani anayotokana na Chama hicho Ally Sharif pamoja na mgombea urais Bernard Membe, ifikapo mwezi Oktaba 28 mwaka huu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment