Na Yassir Simba, Michuzi Tv
Mchezo namba sita ulioasharia kufunguliwa kwa pazia la ligi Kuu Tanzania bara VPL 2020/2021,uliwakutanisha Young Africans dhidi ya maafande wa Jeshi la magereza Tanzania Prisons.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya 7:00 usiku, ulishuhudia Young Africans wakipata sare ya kufungana bao 1 -1 katika uwanja wa nyumbani dhidi ya wenyeji wa mchezo huo Tanzania Prisons.
Alikuwa na Lambert Sabiyanka aliyeanza kuipatia bao la kuongoza Tanzania Prisons katika dakika ya 8 ya mchezo mara baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 liliyomshinda mlinda mlango wa Yanga Farouk Shikalo, Huku ikiwalazimu Young Africans kusubiri hadi dakika ya 19 ya mchezo kusawazisha bao kupitia mshambuliaji wao wa kimataifa kutoka nchini Ghana Michael Sarpong na kuufanya ubao wa magoli katika dakika 45 za kipindi cha kwanza kusomeka 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Young Africans wakifanya mabadiliko kwa kumtoa Farid Musa pamoja Deus Kaseke huku nafasi zao zikichukuliwa na Tuisila Kisinda pamoja na Yacouba huku Zawadi Mauya akimpisha Mukoko Tonombe katika nafasi ya kiungo.
Young Africans walikuja na adhma ya kulisakama lango la Tanzania Prisons ambapo kupitia winga wao Tuisila Kisinda walitengeneza nafasi kibao ambapo walishindwa kuzitumia huku presha ya mchezo ikiwa juu kwa Tanzania Prisons ambapo dakika 81 ya mchezo beki kisiki wa Prisons Nurdin Chona alizawadiwa kadi nyekundu na muamuzi wa mchezo huo Emmanuel Mwandemba na kuwafanya Prisons kucheza pungufu hadi dakika 90 ya mchezo.
Rasmi Young Africans anabaki nafasi ya sita katika msimamo wa ligi akiwa nyuma kwa alama mbili dhidi ya kinara wa ligi Simba Sports Club ambaye jana katika dimba la Sokoine jijini Mbeya, aliwakaribisha wageni wa ligi hiyo timu ya Ihefu kwa kipigo cha mabao 2-1 mabao ya John Bocco katika dakika ya 11, bao la Mzamiru Yassin dakika 43 huku Ihefu wa kufuta machozi kwa bao la Omary Mponda dakika ya 15 ya mchezo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment