Na Samwel Mtuwa - GST.
Leo Septemba 7 , 2020 wataalam kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Idara ya Jiolojia wampatia Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Budeba kitabu maalum aina ya Notebook kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Utafiti wa jiosayansi.
Akizungumza wakati wa kumkabidhi Notebook hiyo Mkuu wa Idara ya Jiolojia katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt.Elisante Mshiu alielezea juu ya ubora wa kitabu hicho ikiwa pomoja na kuwepo na mchoro wa rula kwa ajili ya kufanya vipimo vya skeli za Jiosayansi , kila kurasa yake ina sehemu ya kuonesha hali ya hewa ya siku husika ya kazi ikiwa pamoja na kurasa kuwa na sehemu mbili maalum kwa ajili ya uandishi na uchoraji.
Akiwa katika mazungumzo maalum na wataalam hao Mtendaji Mkuu wa GST Dkt.Mussa Budeba alisema kuwa kwasasa GST imejipanga vizuri katika kutekeleza majukumu yake na inataka kujiendesha kisasa zaidi ili kuleta tija kwa taifa ikiwa pomoja na kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na tekinolojia kama taasisi zingine duniani.
Mapema baada ya kupokea Notebook Dkt.Budeba aliwashukuru wataalam hao na kuwaahidi kuwa wataalam wa GST watapata fursa ya kutumia Notebook hiyo wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya shughuli za ugani ambazo huwa zinafanyika kila mwaka ambazo ni maalum katika utendaji wa kazi zao.
Dkt. Mshiu aliongeza kuwa Notebook hii ina kurasa zaidi ya mia mbili na ina uwezo wa kutunza taarifa za ugani kwa zaidi ya miaka ishirini na kuhusu umiliki wa Notebook hiyo Dkt. Mshiu alisema kuwa baada ya kutumiwa na mtaalam itabaki kuwa mali ya taasisi ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu mojawapo juu ya taarifa za jiosayansi kutoka eneo husika.
Wakizungumzia juu ya shughuli za ugani zinazofanywa na GST wataalam hawa wamempongeza Dkt.Budeba kuwa shughuli za ugani zinafanyika kwa tija kutokana na mfumo mpya wa kutoa mrejesho wa matokeo ya utafiti katika eneo husika.
Timu hii ya Wataalam watatu imeongozwa na Dkt Elisante Mshiu ambaye ni Mkuu wa Idara ya Jiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dkt. Charles Kasanzu ambaye ni mwadhiri mwandamizi na Dkt . Emmanuel Kazimoto.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment