Baadhi ya Watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakipatiwa mafunzo ya mfumo wa madeni ya Watumishi Serikalini unaojulikana kama MADENI MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM (MadeniMIS) ambao una lengo la kuhakiki na kuthibitisha madeni ya watumishi.
……………………………………………………….
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili wilayani Busega katika ukumbi wa shule ya Msingi Nyashimo (TRC). Mafunzo haya yameanza kutolewa jana tarehe 8 Septemba, 2020.
Mfumo wa MadeniMIS utatumika kuratibu madeni na madai ya Watumishi wa Serikali yasiyo ya mshahara kwa nchi nzima lakini kwa kuanzia utaanza na madeni ya Walimu, alisema mwezeshaji wa mafunzo hayo, Ndg. Sweetbert Kashaija kutoka TAMISEMI. Lakini pia mfumo huu utapunguza malalamiko ya madai na madeni kwa Watumishi wa Serikali.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment