Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.
SHIRIKA la ndege la kimataifa la Emirates limeendelea kuongeza maeneo ya huduma za usafiri wa anga barani Afrika kwa kufikia maeneo 15 zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo imeelezwa kuwa safari za Luanda, Angola zimeanza Oktoba Mosi, na kuelezwa kuwa safari za Luanda Dubai zitakua mara moja kwa wiki kupitia ndege za EK793 na EK794.
Imeelezwa kuwa Emirates inaendelea kuhakikisha inafikia mahitaji ya wateja wao ulimwenguni kote na hasa kwa kipindi hiki ambacho Mji wa Dubai umefunguliwa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo biashara za kimataifa na utalii.
Aidha imeelezwa kuwa Shirika hilo linaendelea kuhakikisha usalama kwa wasafiri, wageni na jamii kwa kuwapima Covid-19 wasafiri wote wanaowasili Dubai na UEA wakiwemo raia wa UEA, wasafiri na watalii bila kujali nchi walizotoka.
Imeelezwa, kupitia Emirates abiria wanaotoka Dubai wanaweza kupata vipimo vya Covid-19 wakiwa mbali na nyumbani ndani ya saa 48 pekee bila malipo na kuweza kusafiri kwa uhuru, amani.
Aidha imeelezwa kuwa Emirates bado inasimamia sera zao kwa kuwapa wateja machaguo zaidi katika kubadili safari walizopanga na kuingiliwa na mlipuko wa virusi vya Corona.
Dubai ni moja ya kivutio pendwa sana ulimwenguni na tafiti zinaonesha kwamba kwa mwaka 2019 pekee, Mji huo ulipokea wageni milioni 16.7 waliotembelea Mji huo kwa shughuli za kibiashara za kimataifa, utalii, mikutano, michezo na burudani pamoja na maonesho mbalimbali.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment