Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo (kushoto) akimkaribisha Mgombe Ubunge Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega. azungumze na wananchi wa kata ya Mkamba.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani,Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi kata ya Mkamba katika mkutano wa kampeni (Picha na Emmanuel Massaka Michuzi Tv)
Mke wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga koa wa Pwani ,Mariam Ulega (kulia) akiwa amepiga magoti mbele ya wananchi wa kata ya Mkamba akiwaomba wakipe Kura Chana cha Mapinduzi.(Picha na Emmanuel Massaka,Michuzi,Tv)
Mke wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga koa wa Pwani ,Mariam Ulega (kulia) akiwa amepiga magoti mbele ya wananchi wa kata ya Mkamba akiwaomba wakipe Kura Chana cha Mapinduzi.(Picha na Emmanuel Massaka,Michuzi,Tv)
Na Mwandishi wetu,Michuzi Tv
WANANCHI wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani wameahidiwa kuwa ndani ya miaka mitano ijayo barabaraba ya Kimanzichana, Mkamba kupitia Vianzi Changendere kwenda kutokea Kisarawe itaendelea kukarabatiwa na kufunguliwa.
Ahadi hiyo imetolewa na mgombea ubunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega wakati wa mkutano wa kampeni aliyofanya katika vijiji vya kata ya Mkamba ambapo ameeleza ujenzi wa barababara hiyo utarahisisha safari kwa wakazi wa Mkuranga wanaotaka kwenda Kisarawe au Kibaha ambao kwa sasa wanalazimika kupitia jijini Dar es salaam.
Aidha Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema katika miaka mitano mikakati ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) na serikali ni kurekebisha na kutanua barabara hiyo ambayo ndio pekee inayounganisha kisarawe na mkuranga na ,zilizobaki zote lazima upitie Dar es salaam .
Ulega ameongeza lengo ni kuhakikisha Mkamba inakuwa kiuchumi kwasababu barabara hiyo ikifunguka wana Mkamba watapata urahisi wa kusafirisha mazao yao kwenda sokoni kwa wepesi kwani wakulima wa mazao mbalimbali yakiwemo mananasi na mihogo.
"Tunamkakati wa pamoja kati yangu mimi na Suleiman Jafo wa Kisarawe kuhakikisha hii barabara inapatikana na inafunguka, nia tunayo na jambo hili tutalifanya lakini naomba ndugu zangu itakapofikia muwe tayari kwa athari zitakazo patikana ikiwa ni pamoja na kukata mikorosho yenu ilituweze kutainua, "amesema Ulega
Vijiji vinne alivyovafya kampeni Ulega ni Kizomla,Tungi,Kigoda na Mkerenzange ambapo kwa pamoja ameviomba kuchagua chama cha mapinduzi ccm ili waweze kutatuliwa changamoto yao ya maji .
Mgombea huyo amesema anajua changamoto kubwa ya maji iliyopo katika kata ya mkamba na inashughulikiwa kwani tayari kuna mradi wa maji wa billion 2.1 utakao sambaza maji katika vijiji hivyo.
Kwa upande mwingine ulega amesema shule ya Msingi Kizomla ni kongwe kwani imeanzishwa mwaka 1977 lakini haijawahi kufanyiwa marekebisho na kwamba atatoa bati za madarasa matatu, pamoja na mifuko ya saruji kwa ajili ya vyoo vya walimu huku akitoa maelekezo ukarabati ufanyike ili ifikapo Januari mwakani watoto wasome vizuri.
Pia amesema kuwa ataimarisha shule ya msingi Tungi kwa kuwapeleka madawati,maabara na kuboresha nyumba ya Mwalimu baada ya ccm kushida uchaguzi mkuu october 28.
Sanjari na hayo Ulega amesema kuwa harakati za umeme zimeshaanza katika kata hiyo na mpaka ifikapo mwezi desemba mwaka huu umeme utakuwa umefika na vijiji vitakavyobakia navyovitapata kupitia umeme waujazilizi.
Hata hivyo mgombea huyo amewapongeza wananchi hao kwa kuimarisha shughuli za kilimo na kuwaahidi kuwasaidia kuondoa wanyama waharibifu wa mazao wakiwemo Ngedere na Nyani.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa Kata ya Mkamba kupitia CCM Hasani Dunda amesema mpaka sasa mgombea urais wao wa urais Dk.John Magufuli ametoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya shule ya msingi Mkamba na kuwaomba wananchi kuendelea kukiunga mkono chama hicho kwa ajili ya mandeleo ya kata huyo na Taifa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment