JOYCE KIRIA AMTEMBELEA MWALIMU ALIYEKATWA KALIO NA MKONO | Tarimo Blog

 


Na Woinde Shizza, Arusha
MWANAHARAKATI na mtetezi wa haki za wanawake nchini Joyce Kiria 'The
Super Woman.' amemtembelea mwalimu Veronica Daudi, aliyekatwa  sehemu za mikono  na makalio na mume wake kwa madai ya wivu wa mapenzi.

Akiongea katika hospital ya Selian iliyopo Ngaramtoni, Wilayani Arumeru
mwanaharakati huyo amesema kuwa, amesikitishwa na tukio hilo la
mwanamke huyo la kukatwa kinyama  mkono na makalio na mume wake wa ndoa akidai mke wake sio mwaminifu katika ndoa yao.

Kiria akiwa katika wodi aliyolazwa mwalimu Veronica Daudi, amewaasa
wanawake kuacha kuvumilia vitendo vya unyanyasaji ambavyo wamekuwa
wakifanyiwa na waume zao na badala yake watoe taarifa kwa vyombo vya
dola ili hatua zaidi zichukuliwe.

Amesema wanawake wengi wamekua wakikosa haki kwa kuvumilia vipigo na
manyanyaso ndani ya ndoa wakihofia kutengana na familia zao jambo
linalo leta madhara makubwa kwa kuchukuliana sheria mkononi.

Joyce ni miongoni mwa wanawake wanaharakati waliojitolea kusaidia
wanawake kupata haki  kupitia kipindi cha 'Wanawake Live' kinacho
zungumzia manyanyaso na ukatili wa wanawake katika jamii.

Kwa upande wake, Mwalimu Veronica Daudi ameshukuru Joyce Kiria kufika
wodini hapo na kumpa faraja pamoja na kumsaidia mchango  wa kuanza
kupata mkono wa bandia na baadae kurejea kazini kwakwe kufundisha
wanafunzi kama mwanzo.

Amesema kilicho pelekea yeye kukatwa mkono na mume wake  ni wivu wa
mapenzi, Na hiyo ni baada ya mume wake kumlalamikia mara kwa mara juu ya kuwa na mahusiano na mwanaume wengine jambo ambalo si la kweli.

Mwalimu Veronica ni mwalimu wa Kingereza katika shule ya sekondari ilkidiga iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, Ameeleza mpaka sasa hajui hatima ya maisha yake ya ualimu kwani ndio ajira anayoitegemea katika kulea familia yake. 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2