Na Emmaul Masaka, Michuzi TV- Mkuranga
MGOMBEA ubunge jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amesema atahakikisha analiinua zao la korosho wilayani Mkuranga ili uchumi wa wananchi wa eneo hilo uinuke.
Akizungumza leo na wananchi wakati wa mikutano yake ya kampeni aliyoifanya katika vijiji vinne vya Nyamihimbo,Mtongani,Nasibugani pamoja na msonga vya Kata ya msonga wilayani Mkuranga mkoani Pwani Ulega amesema yuko tayari kuwaonesha njia wananchi kwa kuwakutanisha na taasisi zakifedha ili wapate pembejeo.
Aidha Ulega ameongeza kuwa anafahamu kuwa korosho ni uhai na ni uchumi hivyo ataendelea kulipambania zao hilo ili kukuza pato la wananchi wa kata ya msonga na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo amesema miaka mitano ijayo anaenda kukarabati barabara ya Nyamihimbo mpaka Mtongani kwa kuweka karavati katika sehemu korofi ili malori yanayobeba korosho yaweze kupita kwa urahisi na mazao yanayolimwa katika kata hiyo yafike sokoni kwa wakati.
Akizungumzia barabara ya Nasibugani kwenda mavunja amesisitiza kuwa pesa ya barabara hiyo imepatikana na tarura inenda kuwekea makaravati nane kabla ya kipindi cha masika kijacho na kuwataka wananchi kuchagua chama cha mapinduzi ili barabara hiyo ipitike kipindi chote .
Kwa upande wa umeme Ulega amesema umeme utafika katika vijiji vyote ikiwemo msambanyamani na mavunja.
Mgombea huyo amesisitiza kmikakati yake mikubwa katika miaka mitano hii ni kuhakikisha anawatoa unyonge wananchi wa kata ya msonga kwa kuwaletea maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu,umeme pamoja na maji.
Pia amesema wanaenda kufanyia ukarabati shule ya msingi Nasibugani ambayo nikongwe kwa kujenga madarasa zaidi ya matano ili watoto wa eneo hilo wapate elimu bora.
Ulega meahidi kutoa mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya kuanzisha zahanati ya Nyamihimbo na kuongeza kuwa miaka mitano iliyopita alishaanzisha zahanati zaidi ya 35 katika vijiji mbalimbali vya Mkuranga kiwemo kijiji cha msonga lengo ni kutatua changamoto za afya kwa wananchi.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani,Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi kata ya Msonga katika mkutano wa kampeni
(Picha na Emmanuel Massaka Michuzi Tv)
Wananchi wakiwa wameshika mabango ya wagombea.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment