MGOMBEA UBUNGE MKURANGA AAHIDIKUSIMAMIA HAKI, MASLAHI YA WAFANYAKAZI | Tarimo Blog

Mgombea wa ubunge Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wanachama wa chama Cha Mapinduzi katika Mkutano Kampeni za Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28, 2020 nchini Kote. 


Wananchi wakimsikiliza mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega.

Na Emmanuel Massaka, Michuzi TV-Mkuranga
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega amesema atakuwa mkali katika kusimamia haki na maslahi stahiki ya wafanyakazi ambao wanafanya kazi katika wilaya ya Mkuranga.

Ulega amesema hayo wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu katika Kijiji cha Kolagwa kilichopo Kata ya Mipeko ambapo amesema katika wilaya hiyo kuna wawekezaji waliowekeza katika viwanda, hivyo Serikali ya CCM itahaiikisha inasimamia haki na maslahi yaliyowekwa baina ya wafanyakazi, vijiji, halmashauri na taifa ili kupata tija.

Amesema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 imeeleza wazi kuhusu haki na maslahi hayo hivyo iwapo wagombea wa CCM watapata kura za ushindi wa kishindo watasimamia hilo.

Amefafanua kwamba Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli ndio anajua wawekezaji hao amewatoa wapi hata wakaja kuwekeza katika mkoa huo wa Pwani, hivyo wachague CCM iliwasimamie haki na maslahi hayo.

Aidha kwa upande wa haki zinazotolewa baada ya mfanyakazi kupata ajali Sh.300,000 au ulemavu kazini kulipwa 800,000, amesema CCM inatambua kiasi hicho ni kidogo watashughulikia kuongeza fidia hiyo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2