Na Samwel Mtuwa - Lindi
MKUU wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi leo ameipongeza na kuishukuru Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kutoa mrejesho wa utafiti wa awali unaoonesha uwepo wa Madini mbalimbali Wilayani Liwale Mkoani Lindi.
Akizumgumza mapema baada ya kumalizika kwa Uwasilishwaji huo Zambi amesema mrejesho huu utasaidia kufahamu juu ya rasilimali Madini zinazopatikana mkoani Lindi ikiwa pamoja na kuongeza fursa za Uwekezaji katika sekta ya Madini.
"Ukweli ni kwamba sekta ya Madini ina mchango mkubwa katika pato la taifa na sisi hapa Lindi tunapopata taarifa Kama hizi tunasikia faraja Sana, nawashukuru sana wataalam kutoka GST"amesema Zambi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Rehema Madenge ameiomba GST kuwasilisha taarifa za Madini katika Wilaya nyingine za Mkoa wa Lindi zinazobainisha uwepo wa Madini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mbwana Kambangwa amesema kuwa utafiti huo wa awali utafungua milango ya uwekezaji katika sekta ya Madini ndani ya Wilaya ya Liwale.
Uwasilishwa wa mrejesho wa Utafiti awali imewakutanisha na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Katibu Tawala Mkoa wa Lindi , wakuu wa vyombo vya ulinzi na usala ma mkoani Lindi , Kamanda wa TAKUKURU mkoani Lindi, watumishi mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na waandishi wa habari.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment